Na Shaban Kondo,
Kamati ya
uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF imeendelea imetoa taarifa ya
kurekebisha orodha ya pingamizi iliyotolewa katika vyombo vya habari kwa
kueleza iliacha pingamizi lililowekwa na Paul Mhangwa dhidi ya Mugisha Galibona
na Vedastus Lufano ambao wanaomba nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF
kupitia kanda ya pili (Mwanza na Mara).
Kamati ya
uchaguzi ya TFF iomeomba radhi kwa pingamizi hilo kuachwa kwenye orodha
iliyotolewa hapo jana katika vyombo vya habari, hivyo imesisitiza wahusika hao
kufika bila kukosa katika kiksoi cha kujadili pingamizi kitakachofanyika
jumatano Januari 30 katika ofisi za TFF kuanzia saa nne asubihi.
Katika
hatua nyingine kamati ya uchaguzi ya TFF imewataka walioweka pingamizi dhidi ya
wagombea nafasi mbali mbali za uongozi wa TFF kuwa na ustahamilivu katika
kipindi hiki kwa ajili ya kuiachia kamati hiyo kufanya kazi yake ipasavyo.
Akizungumza
kwa niaba ya kamati hiyo katibu mkuu wa TFF Angetille Osiah amesema hairuhusiwi kwa yoyote alioweka pingamizi
dhidi ya wagombea kwenda katika vyombo vya habari na kuliweka wazi pingamizi
lake.
0 comments:
Post a Comment