Siku mbili
baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu ambao utamuwezesha kuwepo
Emirates Stadium hadi mwezi June mwaka 2016, mshambuliaji Theo Walcott ametoboa siri ya kukamilisha mpango huo.
Walcott ambae alizusha hofu kwa viongozi na mashabiki
wa klabu ya Arsenal kutokana na kuonyesha hali ya kugomea mchakato wa kusaini
mkataba huo mwanzoni mwa msimu huu, amesema siri kubwa ya kusaini mkataba mpya
ni kutimizwa kwa matakwa yake ya kutaka kuchezeshwa kama mshambuliaji wa kati.
Amesema
anaamini suala hilo litazingatiwa japo halitokua la kudumu, kutokana na mfumo
utakaokuwa unatumiwa na meneja Arsene
Wenger pale itakapohitajika kufanywa hivyo.
Naye, mshambuliaji kutoka nchini Argentina
Carlos Tevez amesema alikaribia
kufanya maamuzi ya kustahafu mchezo wa soka, kufuatia ugomvi wake na meneja wa
klabu ya Man city Roberto Mancini uliojitokeza
msimu uliopita.
Carlos Tevez
mwenye umri wa miaka 28 amesema alikuwa katika mazingira magumu na wakati
mwingine alidiriki kujifungia chumbani na kulia huku akujilaumu na kikitafsiri
kitendo hicho kama mkosi uliokua umemkuta katika maisha yake ya soka.
Hata hivyo amesema alifikia maamuzi
ya kujirekebisha yeye binafsi kabla ya
kuamua kurejea mjini Manchester na kuomba radhi kutokana na kosa alilolifanya
na kisha kujiunga na wengine, hatua mbayo iliwasaidia wote kwa ujumla na
kufanikisha azma ya kutwaa taji la Uingereza msimu uliopita.
Carlos Tevez
alizusha sakata hilo, baada ya kugoma kupasha misuli moto wakati wa mchezo wa
hatua ya makundi wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC
Bayern Munich msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment