Chanzo:- Bomba FM 104.0MHz
Chama cha wendesha bajaji
mkoani Mbeya kimetoa misaada mbalimbali katika kituo
cha kulea watoto yatima cha
malezi na huruma kilichopo katika eneo la simike kwa lengo la kurudisha
shukrani kwa wateja wake
Akizungumza na bomba
fm mwenyekiti wa chama hicho Idd
Ramadhani amesema wamejiwekea mfumo wao kama chama cha bajaji kwa kufuata nyayo
za mlenzi wa chama hicho Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo ili kuweza
kuwasaidia wasiojiweza na kwamba kila wanajamii anapaswa kuguswa na kujitokeza
kutoa misaada .
Kwa upande wake katibu wa bajaji Ernest Mwaisangu ameseviasa vikundi mbalimbali kuweza
kujipanga na kuweza kutoa misaada kwa wasiojiweza kuifahamisha serikali mambo muhimu ambayo
yanafanyika katika kuisaidia jamii .
Kwa upande Frank Musa mmoja wa watoto hao
ametoa shkrani kwa chama hicho na kuwaomba kutokukata tama kuwasaidia
ili nao waweze kuwasaidia wengine walitoa shukwani.
Aidha, kituo cha hicho kupitia mmoja wa walezi, kimetoa
shukrani zake za dhati kwa umoja wa waendesha bajaji kwa kitendo cha kuwapatia
misaada mbalimbali kituoni hapo.
Hata hivyo mdau mkuu wa umoja wa wandesha bajaji hao Noah Mwakisu vikundi vingine ili kuwapa hamasa zaidi na
amevitaka vikundi vingine kuiga mfano kama huu waliouonyesha umoja wa
bajaji kwa kutoa misaada katika jamii
0 comments:
Post a Comment