Na mwandishi wetu.
Askari polisi saba wa kituo cha polisi
Mbozi wanatuhumiwa kwa kumpiga, kumjeruhi na kumsababishia maumivu makali Laiton
Mwakalinga mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Kijiji cha Haterere.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Laiton
Mwakalinga alipigwa na askari wakati akipeleleka malalamiko dhidi ya shemeji
yake aliyemtishia kumuua ambapo askari hao walimtaka atoe kiasi cha shilingi elfu
arobaini na alipogoma ndipo walipoanza kumpiga hadi kumvunja mkono.
Kutokana na kitendo hicho Kamanda wa polisi
mkoani hapa Diwani Athumani ameahidi kulifuatilia tukio na kutoa wito kwa
wananchi kuendelea kutoa taarifa haraka na zenye ukweli ili tatizo kutafutiwa
ufumbuzi ili kupatikana kwa haki sawa kwa raia na vyombo vya usalama.
Aidha amesema kitendo cha askari kumpiga
raia ni kosa na halitakwi kufumbiwa macho na kwamba askari kuwakamata raia na kuwapiga sio utaratibu na haipo katika
utaratibu wa upelelezi wa jeshi hilo nani kosa la jinai na lisichukuliwe kama
ni utaratibu wa Polisi bali ni wa mtu binafsi askari mmoja mmoja kujichukulia
umamuzi.
0 comments:
Post a Comment