Pages


Home » » Mtoto afariki dunia kwa ajali ya Moto...

Mtoto afariki dunia kwa ajali ya Moto...

Kamanga na Matukio | 03:02 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
 Mtoto Halaika Bushiri (7) mwanafunzi wa shule ya msingi Mwanyanje iliyopo kata ya Igawilo jijini hapa amefariki dunia baada ya kuketea kwa moto akiwa nyumbani kwao jana majira ya saa 7:45 ya mchana, Januari 21 mwaka huu.



Shuhuda wa tukio hilo Recho Jeseph (36) amesema mtoto huyo aliza kupiga kelele za kuomba msaada mara baada ya kutokea kwa moto wakati mama wa mtoto Nuru Mlele akiendelea shughuli zake licha ya majira kujitokeza na kuuzima moto huo.



Katika hali ya kushangaza mama huyo hakuonesha kustushwa na kitu chochote na wakati tukio hilo aliendelea kufua nguo, hadi pale majirani walipofanikiwa kuudhibiti moto huo ambao uliteketeza samani za nyumba yake ikiwemo seti moja ya kochi na.



Aidha kutokana na juhudi za majirani kushirikiana ndani ya dakika kumi walifanikiwa kuudhibiti moto huo na kuuzima lakini mtoto huyo alikuwa tayari ameshafariki.

Hata hivyo licha ya polisi kupewa taarifa majira ya saa tisa kamiliwalifika majira ya saa kumbi na mbili na robo jioni, eneo la tukio lenye umbali wa mita mia sita kutoka kituoni, hali iliyowasononesha sana wananchi.



Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger