Chama cha madereva bajaji mkoani Mbeya
kimedhamiria kurejesha shukrani zake kwa wateja wake kwa makundi maalum kwa
kutoa misaada mbalimbali
Mwenyekiti wa chama hicho Idi Ramadhan amesema kwa kuanza chama hicho kitawatembelea
watoto yatima katika kituo cha Isalaga kilicho Uyole Mbeya na zoezi hilo litafanyika kila mwisho wa
mwezi.
Wakati huohuo amewataka vijana
kuungana kwa pamoja katika kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuondokana na tabia
ya kukaa vijuweni huku wakilalamika tatizo la ajira.
Aidha ameiomba Serikali
kutimiza dhamira yake ya kusaidia vijana kwa vitendo ili waweze kuondokana na
vitendo vya uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya.
0 comments:
Post a Comment