Bwana Fredrick Mwakalebela aliekua Katibu Mkuu wa TFF
Aliekua katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF
Fredrick Mwakalebela amezungumzia uchaguzi wa shirikisho hilo kwa kuitazama
nafasi ya uraisi inayoonekana kutoa upinzani kwa Jamali Malinzi pamoja na
Athumani Nyamlani ambae kwa sasa ni makamu wa kwanza wa raisi.
Mwakalebela ambae alitenda kazi zake kwa uadilifu mkubwa
akiwa TFF kabla ya kutangaza kuaiacha nafasi ya ukatibu na kuingia katika
masuala ya kisisa mwaka 2010, amesema licha ya kuwepo kwa mgombea Omary Mussa Nkwarulo
katika nafasi ya uraisi, bado anaona upinzani mkubwa bado upo kwa Jamali
malinzi pamoja na Athumani Nyamlani.
Hata hivyo Fredrick Mwakalebeka akawataka wajumbe wa TFF
kutumia nafasi yao ya kupiga kura kwa uadilifu mkubwa kutokana na hitaji la
soka la bongo ambalo kwa sasa lina hamu ya kupata mafanikio kama ilivyo kwa
nchi nyingi barani Afrika na kwingineko.
Wakati huo huo Uongozi wa chama chama cha makocha wa soka TAFCA mkoa wa
umeyapokea kwa mikono miwili maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya TFF ya
kuuahirisha uchaguzi wa chama hicho taifa uliokua umepangwa kufanyika JAnuari
19 jijini Dar es salaa.
Katibu mkuu wa TAFCA Abubakari saidi Behengula amesema
pamoja na maamuzi hayo kuchelewa kutplewa kwa wakati bado anaamini TAFCA
itapata nafasi ya kujipanga upya na kufuata taratibu za kikatiba kwa ajili ya
kukamilisha uchaguzi mkuu ambao umeamishwa kufanyika baada ya uchaguzi wa TFF.
Hata hivyo Saidi Behengula akaendelea kuzungumzia jambo
linguine ambalo kwa upande wa Mwanza wameliona ni la busara zaidi baada ya
kuutumia mkutano wa uchaguzi wa TAFCA kuwa kama mkutano mkuu wa kujadili agenda
mbali mbali.
Amesema suala kubwa lillilomfurahisha ni kukubaliana kwa
pamoja kuwa uongozi wa TAFCA taifa uliopo madarakani kupewa ridhaa ya kuendelea
na kufuta kasumba ya kuunda kamati ya muda ya uongozi.
0 comments:
Post a Comment