Pages


Home » » WANACHUO WAGUSHI MUHURI WA BENKI, WATAFUNA ADA MILIONI 12 MKOANI MBEYA.NA

WANACHUO WAGUSHI MUHURI WA BENKI, WATAFUNA ADA MILIONI 12 MKOANI MBEYA.NA

Kamanga na Matukio | 06:34 | 0 comments
Wanachuo 33 wa chuo cha Ilemi Polytechnic College wamefuja shilingi milioni 12, 450,000 za kitanzania, ada ambazo walipasa kulipa kwa ajili ya mafunzo wanayopatiwa katika chuo hicho kilichopo kata ya Iganzo jijini Mbeya.

Wanachuo hao badala ya kwenda kulipa ada hizo katika akaunti ya malipo ya shule katika Benki ya Exim, wamekuwa wakichukua stakabadhi ya malipo (pay slip) na kuzigonga muhuri ambao wameuchonga, kisha kuzipeleka stakabadhi hizo kwa mhasibu wa chuo hicho kama malipo halali ya ada.

Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto wa kike waliofanya udanganyifu huu, ambapo baada ya kubanwa na uongozi wa Benki ya Exim na chuo hicho waliweza kukiri kufanya udanganyifu huo.

Hata hivyo katika udanganyifu huo Benki hiyo haijaweza kuathiriwa na kitu chochote kwani pesa zote zipo salama, na kwamba wanafunzi hao wameathiriwa kwa asilimia kubwa kutokana na kutafuta ada zao.

Akizungumza na mtandao huu Mkuu wa chuo hicho Bwana Bon Beny Mwasaka amesema kuwa wanachuo waliofanya udanganyifu huo ni wanachuo ambao wamejiunga na masomo kwa mwaka wa kwanza, kwani chuo hicho hakijaweza kupata hasara yoyote kutokana na wengi wao kudaiwa ada na kuanza kulipa huku uchunguzi ukiendelea kufanyika ili kuweza kubaini mmiliki wa mhuri huo bandia.

Amesema kuwa wanachuo hao wameweza kugushi nyaraka za malipo ya ada kuanzia laki moja hadi laki nne na elfu themanini na kwamba atakayekamatwa kuhusika na tukio hilo la udanganyifu atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa chuo.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Exim Bwana Godfrey Kitundu amesema wamebaini kasoro zaidi ya 14 za muhuri huo, ambazo zimeonekana katika mhuri huo hivyo haikuwa rahisi benki hiyo kudanganywa na tukio hilo la kugushi nyaraka za malipo, kuwa tofauti zilizopo katika stakabadhi hizo ni pamoja na tarehe za ulipaji kuonesha ni siku ambazo benki haikufunguliwa ikiwemo Novemba 11, ambapo kulikuwepo na tukio la vurugu eneo la Mwanjelwa kutokana na benki hiyo kuwa karibu na eneo hilo pamoja na siku za jumapili.

Hata hivyo ametoa ushauri kwa chuo hicho kufuatilia mara kawa mara maendeleo ya akaunti yao ya chuo ili kubaini mapema matatizo kama hayo yaliyojitokeza na kwamba wataendelea kutoa ushauri mara kwa mara ili kuhakikisha pesa za chuo zinakuwa salama.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa chuo hicho Bwana Elton Mwamasika amewataka wanachuo kulipa mapema kiasi cha ada wanachodaiwa, endapo watachelewesha ulipaji huo basi huenda wakasimamishwa kuendelea na masomo, lakini mtandao huu uliweza kushuhudia wanachuo hao wakilipa da zao ka kuruhusiwa kuingia katika vyumba vya mitihani.

Chuo hicho hutoa mafunzo ya kilimo, biashara na kompyuta(ICT) kwa gharama ya shilingi laki 7 ambazo ni gharama za kila mwanachuo mmoja kwa hatua ya cheti na diploma.





Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger