Pages


Home » » HALI SI SHWARI NCCR - MAGEUZI MBEYA

HALI SI SHWARI NCCR - MAGEUZI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:58 | 0 comments
 Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi wilaya ya Mbeya Bwana Andulile Mwakibete Kapaga akizungumzia msimamo wa chama chake kuwa viongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi, madiwani , wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa pamoja na wanachama wa chama hicho mkoani Mbeya wamesema wanamtambua na kumkubali Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Mheshimiwa James Mbatia pamoja na viongozi wake wa ngazi za Taifa.
  Baadhi wa wajumbe wa chama cha NCCR - Mageuzi aliohudhuria mkutano wa chama hicho juu ya msimamo wao kuwa viongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi, madiwani , wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa pamoja na wanachama wa chama hicho mkoani Mbeya wamesema wanamtambua na kumkubali Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Mheshimiwa James Mbatia pamoja na viongozi wake wa ngazi za Taifa.
*****
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Viongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi, madiwani , wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa pamoja na wanachama wa chama hicho mkoani Mbeya wamesema wanamtambua na kumkubali Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Mheshimiwa James Mbatia pamoja na viongozi wake wa ngazi za Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya Bwana Andulile Mwakibete Kapaga ameserma kuwa wanalaani na kukanuusha kwa nguvu tamko lililotolewa gazetini kuwa kikao cha chama hicho mnamo Novemba 30, mwaka huu kilidai kuwa Wenyeviti wa majimbo NCCR- Mageuzi wamkataa Mwenyekiti wao wa Taifa Mheshimiwa James Mbatia 

Amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya  chama cha NCCR- Mageuzi, hakuna kikao chochote cha kimkoa na kwamba kikao hicho kilikuwa ni batili na hivyo ndugu Lobson Fongo hakuwa na uhalali wa kujiita mwenyekiti wa chama hicho mkoa na kutoa tamko kwa niaba ya wenyeviti wengine wa wilaya nyingine za mkoa huu.

Bwana Andulileameongeza kuwa chama cha NCCR - Mageuzi mkoani hapa hakina imani na Kamishna wa chama hicho mkoa Bwana Daimon Mwampeta kwa kuitisha kikao kisicho halali na kisichofuta katiba ya chama hicho.

Ameongeza kuwa wanaomba wananchi watambue kuiwa chama hicho ni chama tulivuchenye viongozi katika umma kama madiwani, wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger