Pages


Home » » MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU, HOSPITALI TEULE YA IFISI - MBEYA VIJIJINI YAPIGA HATUA.

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU, HOSPITALI TEULE YA IFISI - MBEYA VIJIJINI YAPIGA HATUA.

Kamanga na Matukio | 05:59 | 0 comments
Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali TACOMO Bwana Gordon Kalulunga alipotembelea wadi ya watoto Hospitali teule ya Ifisi iliyopo miji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini kuwajulia hali katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.
Muuguzi mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi iliyopo mji mdogo wa Mbalizi Bi Rhoda Kasongwa(kushoto), akipokea maelezo ya Muuguzi wa wadi ya watoto Bi Atu Mwasumbi(63), baada ya kutembelewa na Asasi isiyo ya kiserikali TACOMO  Hospitali hapo kuwajulia hali wagonjwa katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.
 Bendera ya Taifa ikiashiria kufana kwa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo mji mdogo wa Mbalizi, mbeya vijijini ambapo mikoa ya Nyanda za juu kusini imekuwa ikinufaika kwa kupata tiba bure ya magonjwa sugu kama vile kansa, kifua kikuuu na midomo sungura kwa rika zote.






Gari la kubebea wagonjwa linalokokotwa na ng'ombe vijijini, kwa kuwapeleka wagonjwa wasiojiweza hospitalini kupatiwa matibabu.
*****
 HOSPITALI teule ya wilaya ya Mbeya Vijijini inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, imesema kuwa wananchi wamepata elimu na kujua umuhimu wa kupata vipimo vya magonjwa yanayowasumbua kabala ya kupewa dawa na wataalam wa masuala ya Afya.

Hayo yameelezwa jana na Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Rhoda Kasongwa katika kilele cha maazimisho ya miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanzaganyika yaliyokuwa yamefanyika katika Hospitali hiyo kama ishara ya kuunga mkono Serikali.

''Mafanikio makubwa yamepatikana ndani ya miaka hiyo hasa katika suala zima la Afya ambapo awali wananchi walikuwa wakipata dawa bila kupata vipimo lakini kwa sasa hawachukui dawa bila kupimwa na huwa wanadai vipimo kwanza'' alesema Kasongwa.

Alisema kuwa katika kuazimisha kilele cha miaka hiyo ya uhuru, Hospitali hiyo imepata maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja na Hospitali hiyo kujengwa ndani ya miaka hiyo ambapo awali ilikuwa kituo cha Afya kilichokuwa kikihudumia wanafunzi waliokuwa wanapata majeraha ya vidonda katika chuo cha Ufundi Mbalizi.

Kasongwa anasema kuwa hospitali hiyo ina uwezo wa kulaza wagonjwa 200 kwa siku ambapo licha ya kuwa Hospitali pekee katika wilaya hiyo ya Mbeya vijijini tangu uhuru, inahudumia wagonjwa kutoka zaidi ya mikoa mitatu nchini.

Anaitaja mikoa ambayo wagonjwa wamekuwa wakitoka na kufika katika hospitali hiyo kuwa ni pamoja na mkoa wa Tabora, Rukwa, Iringa, Ruvuma pamoja na mkoa wa Mbeya na wilaya zake kwa ujumla.

''Mafanikio haya ni kutokana na huduma tunazozitoa ingawa awali baada ya kuwa na ubia na Serikali wananchi walidhani kuwa huduma zisingeendelea kuwa nzuri lakini ukweli ni kwamba Serikali haitoi huduma mbaya za Afya bali mtaalam mmoja mmoja ndiyo anaweza kulaumiwa hivyo tunajivunia mafanikio haya ndani ya hii miaka'' alisema Muuguzi huyo mkuu.

Kwa upande wake Muuguzi wa zamu katika wodi ya watoto Faines Nunule alisema kuwa baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na kuhudumia wagonjwa wa Ukimwi ambao wazazi wao huficha kiini cha magonjwa ya watoto hao na zaidi alilalamikia ufinyu wa chumba cha kutolea ushauri nasaa ndani ya wodi hilo.

Naye Valelia Benedict alisema kuwa ni muhimu ndani ya miaka 50 hii ya uhuru wa Tanganyika wauguzi wakafuata maadili ya taaluma zao kwa kutoa huduma bila kuwanyanyapaa wagonjwa ambao wengi wao wanahitaji faraja kutoka kwa wauguzi na waganga.

''Kutukana wagonjwa siyo maadili yetu na ninashukuru hapa kwetu hakijajitokeza kitu kama hicho lakini kama wapo popote pale ni muhimu wakajirekebisha kwasababu wagonjwa wanapofika katika Hospitali wanategemea kuapa matibabu na wala si malumbano na wataalam'' alisema muuguzi huyo.

Kwa upande wao wagonjwa waliohojiwa walisema kuwa Hospitali hiyo imekuwa kimbilio kutokana na kuwepo uongozi madhubuti ambao unaruhusu kupokea malalamiko kwa dosari zinazojitokeza na kuwa mstari wa mbele kutoa huduma wenyewe pindi mgonjwa anapokuwa hana imani na muuguzi yeyote wanayeonekana kutofautiana naye.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger