Mtoto Oscar Oliver (17), mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya akiwa ndani ya ofisi za Jeshi la Polisi zilizopo Kituo cha Kati Mbeya, baada ya kuchomwa kiganja cha mkono wake wa kushoto na kaa la moto na mjomba wake kwa kile kinachodaiwa kuwa mtoto huyo kakosa adabu.
Mjomba wa mtoto Oscar Oliver, akiwa tayari kutiwa mikononi mwa Polisi baada ya kubainika kumuunguza kiganja cha mkono wa kushoto mtoto huyo kwa madai kakosa adabu.
*****
Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya
Mtoto Oscar Oliver (17) mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya amechomwa na kaa la moto kiganja cha mkono wa kushoto na mjomba wake kwa tuhuma za kukosa adabu.
Tukio hilo la kinyama limetokea usiku wa kuamkia siku ya sikukuu ya Kristmas nyumbani kwa Andendekisye Mwakabubu (30) ambaye ndiye anayedaiwa kufanya unyama huo kwa mpwa wake akimtuhumu kuwa alitaka kumwibia.
Mwakabubu anadaiwa kumlazimisha mtoto huyo kushika kaa la moto na baada ya mtoto huyo kuungua kiganja chake alimpeleka katika kituo kidogo cha polisi cha Mwanjelwa na kumfunmgulia kesi ya wizi wa kuibiwa vitu mbalimbali ili kuweza kuficha unyama wake huo.
Baada ya kufungua kesi hiyo, askari polisi walimshikilia kijana huyo na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi mkoani hapa na kumweleza mlalamikaji huyo bandia kuwa alitakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mtoto huyo kupelekwa mahakamani.
Mtoto huyo alipofikishwa katika kituo hicho kikuu alikutana na askari waliopo ndani ya kitengo cha kuelimisha jamii kuhusu unyanyasaji wa kijinsi hususani kwa watoto ambao walimsikiliza mtoto huyo na hatimaye jana walimwita mpwa wake kwa ajili ya kutoa maelezo.
Mwakabubu baada ya kufika kituoni hapo na kutoa maelezo na kuulizwa kuwa nani aliyehusika na tukio hilo alishindwa kubainisha huku akisema kuwa hajui aliyemchoma huku akisahau kuwa katika maelezo yake ya awali yeye ndiye alikuwa mlalamikaji jambo ambalo liliwashawishi askari hao kumakamata na kumpeleka rumande.
Mpwa huyo wa mtoto Oscar akiwa mahabausu ya kituo hicho cha polisi, askari hao wanaunda mtandao huo wa kuelimisha jamii juu ya unyanyasaji wa kijinsia mkoani hapa hususani kwa watoto walimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Mwakabubu alihojiwa na askari wa mtandao huo wakiongozwa na askari aliyefahamika kwa jina la Pudensiana Baito huku mwandishi wa habari hizi akiwa anafuatilia tukio hilo na askari huyo alipotakiwa kueleza kwa undani tukio hilo alisema kuwa yeye si msemaji wa jeshi la polisi.
0 comments:
Post a Comment