Pages


Home » » NMB MBEYA YATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IKUTI - MBEYA

NMB MBEYA YATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IKUTI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:53 | 0 comments
Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa misaada ya maguni 112 ya mahindi, maharage magunia 23 na mafuta ya alizeti lita mia tatu, kwa waathirika wa mafuriko wa mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga jijini Mbeya.

Akikabidhi msaada hauo Meneja wa Benki hiyo Bwana Nazareth Lebi, mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama na Mbunge wa Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi, amesema msaada huo umegharimu shilingi milioni 10 za kitanzania na kwamba benki yake inawathamini na kuwajali wateja wake.

Ameongeza kuwa benki hiyo inashirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali yakiwemo majanga, elimu na michezo kwani fedha zinazotolewa ni sehemu ya faida wanayoipata, hivyo wanawarudishia wananchi katika matukio mbalimbali na wananchi wa Ikuti ni sehemu ya wateja wao.

Bwana Nazareth amezitaka asasi nyingine ziendelee kutoa msaada kwa wananchi hao kwani athari yake ni kubwa hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kutokana na kipindi hiki kigumu kutokana na wananchi hao kushindwa kulima na kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi kutokana na baadhi yao kukosa sehemu za kuishi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Bwana Evansi Balama akipokea msaada huo ameishukuru benki hiyo kwa moyo wa uzalendo wa kuwajali wateja wake.

Naye Mbunge wa jimbo la Mbeaya Mjini Bwana Joseph Mbilinyi ameishukuru benki ya NMB kwa kuwathamini wananchi na kujali janga la mafuriko ambalo huathiri kwa kwa kiasi kikubwa shughuli za kimaendeleo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger