Pages


Home » » MUJATA - JESHI LA POLISI HALIWEZI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU BILA KUSHIRIKIANA NA JAMII

MUJATA - JESHI LA POLISI HALIWEZI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU BILA KUSHIRIKIANA NA JAMII

Kamanga na Matukio | 06:27 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu
Chama cha Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kimesema kuwa Amani na utulivu kamwe haiwezi kudumishwa na jeshi la polisi pekee bali ni kwa ushirikiano kutoka kwa jamii.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa MUJATA Chifu Shayo Soja wakati wa mahojiano ofisini kwake na kuongeza kuwa jeshi la polisi halina budi kusimamia nidhamu ya askari wake ambao wamekuwa wakitenda kazi zao bila kufuata misingi ya jeshi hilo.

Aidha ametoa ushauri kwa jeshi la polisi kuunda Sera moja ya ulinzi itakayotumika Tanzania bara na visiwani ambayo pia itafikishwa kwa wananchi na kuwaeleza umuhimu wa wao kushiriki katika ulinzi.

Wakati huohuo amevita vyama vya siasa kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya kidemokrasia badala ya kutumia mwanya huo wa demokrasia kusababisha vurugu na kujenga matabaka hapa nchini.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger