Picha ni mmoja wa wanafunzi walioguswa na zoezi la uchangiaji wa damu salama, kutokana na Benki ya damu ya nyanza za juu kusini kukabiliwa na upungufu mkubwa wa damu.
*****
Habari na mtandao huu.
Benki ya damu kanda ya nyanda za juu kusini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali ambayo inahatarisha usalama wa maisha hasa kwa akina mama wajawazito na wagonjwa wanatoakanao na ajali ambao wamekuwa wakihitaji damu kwa wingi.Akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake meneja wa benki kuu ya kuchangia damu kanda ya nyanda za juu kusini dokta Baliyima Lelo amesema kuwa benki hiyo inaupungufu wa chupa mia moja za damu salama.
Amesema benki hiyo huitaji chupa mia tatu kila siku za damu salama lakini kwa sasa benki hiyo ambayo husambaza damu katika hospitali zote za mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini imekuwa ikipata lita 200 za damu salama badala ya mia tatu.
Kutokana na tatizo hilo Dokta Lelo ameiomba jamii kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha kwa wagonjwa wenye uhitaji mkubwa wa damu hasa kwa akina mama wajawazito ambao mara nyingi wamekuwa wakionekana kuwa na upungufu wa damu mwilini.
0 comments:
Post a Comment