Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Juma Idd(kushoto), akizungumza na Diwani wa kata ya Uyole baada ya kata yao kukumbwa na mafuriko makubwa baada ya mvua iliyonyesha jana, kudumu kwa muda wa saa moja kuanzia majira ya saa kumi hadi za kumi na moja za jioni.
Mafuriko hayo yamesababisha nyumba kadhaa kubomoka na baadhi ya wananchi kukosa hifadhi na kuathiri kambi ya Wachina waliopo jijini hapa kwa ajili ya ujenzi wa barabra ambapo baadhi ya magari yao nusura yabebwe na maji ya mafuriko hayo.
HITIMISHO:- Hata hivyo imeelezwa chanzo cha mafuriko hayo kinatokana na miundombinu mibovu ambapo wakala wa Barabara TANROADS kushindwa kudhibiti hali hiyo kwa muda mrefu licha ya kusisitizwa kupanua na kurekebisha mifereji ya kupitishia maji kiurahisi, pia kilimo kinacholimwa katika eneo la Igawilo kimeendelea kufunga mifereji ya asili ya kupitishia maji.
Wakati huo huo wataalamu kutoka kitengo ya mipango miji, TANROADS, maafa jiji na wilaya ya Mbeya, wanatarajiwa kutembelea Kata hiyo ilikuweza kutathimini hasara zilizotokea hapo jana katika mafuriko hayo.
0 comments:
Post a Comment