Pages


Home » » MISAADA YAENDELEA KUTOLEWA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO - MBEYA.

MISAADA YAENDELEA KUTOLEWA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 06:13 | 0 comments
Mvua kumbwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi na msaada wa haraka wa vyakula na madawa unahitajika ili kuweza kunusuru maafa. Mbali na nyumba kubomoka mvua hiyo iliyodumu kwa muda wa masaa mawili imeweza kuharibu mimea ya mazao shambani. miundombinu ua Maji, Umeme na Barabara kutokana na mafuriko.
Vitongoji vilivyoathiriwa na mvua hiyo katika kata hiyo ni pamoja na kitongoji cha Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 *****
 Habari na Mtandao huu.
Wakazi wa kata ya Ikuti jijini Mbeya waliokubwa na mafuriko disemba 19 mwaka huu wameendelea kupata misaada kutoka kwa wadau mbalimbali ambapo jana mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ameliwapatia msaada wa gunia 40 za mahindi.

Mbunge huyo alikabidhi msaada huo kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyunga, Adia Mwambela chini ya uangalizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Mbeya Ulimboka Mwakilili ambaye alikabidhiwa jukumu la kuwagawia chakula hicho

Mbunge huyo amesema mahindi hayo yametolewa na wakazi wa jiji la Mbeya ambao walihudhuria tamasha la uzinduzi wa albamu yake ya anti vailasi.

Katika tamasha hilo kiingilio kilikuwa ni shilingi elfu tatu na alikuwa ameahidi kutoa shilingi elfu moja katika kila tiketi ili kusaidia watu waliokubwa na mafuriko kata ya Ikuti na kwamba tamasha lake liliingiza shilingi milioni 3 na laki 6

Kwa upande wake afisa Mtendaji wa Kata ya Iyunga, Adia Mwambela alitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa kata ya Ikuti kwa chakula hicho na kuahidi kukifikisha kwa wahusika.
 
Wakati huo huo Benki ya NMB inatarajia kwenda kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger