Pages


Home » » WALIMU WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUTOWACHANGISHA WAZAZIMICHANGO YA MADAWATI - MBEYA

WALIMU WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUTOWACHANGISHA WAZAZIMICHANGO YA MADAWATI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:24 | 0 comments

Afisa Elimu mkoa wa Mbeya Bwana Juma Kaponda akihutubia viongozi na wajumbe waIdara mbalimbali mkoani Mbeya kuhusu mafanikio ya elimu.
*****
Habari na Chanzo Chetu.
Walimu wakuu wa shule za Sekondari za Serikali mkoani Mbeya wametakiwa kuacha mara moja kuwachangisha zaidi ya shilingi Elfu kumi na tano wazazi wa wanafunzi wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza mwaka 2012 kwa ajili ya madawati.

Akijibu swali la mwandishi wa habari hii jana ofisini kwake, juu ya kuwepo kwa wanafunzi kuzuiliwa na kufukuzwa shule wanapoanza kidato cha kwanza wanapokosa kulipiwa na wazazi wao shilingi 30,000, Ofisa elimu wa mkoa wa Mbeya Juma Kaponda, alisema kuwa viwango halisi vya michango ya madawati ni Shilingi 15,000.

Kaponda alisema walimu watakaobainika kuwafukuza wanafunzi waliochaguliwa kwenye shule hizo za serikali mkoani hapa kwa kukosa michango kutoka kwa wazazi wao inayohusu majengo na madawati Serikali haitawavumilia.

‘’Nisema kuwa michango hiyo haikatazwi na Serikali kwasababu shule ni mali ya wananchi lakini michango ya madawati haizidi shilingi Elfu kumi na tano hivyo wananchi wakiona wanatozwa hivyo watoe taarifa kwa maafisa elimu tarafa ama kwa watendaji wao wa kata husika’’ Alisema Kaponda.

Alisema licha ya matokeo ya darasa la saba kutoka na shule kutarajia kufunguliwa Januari 9, 2012 wanafunzi 10,607 hawajapata nafasi kutokana na upungufu wa vyumba 63 vya madarasa.

Mbali na hao Kaponda alisema wanafunzi hao watasubiri katika uchaguzi wa awamu ya pili (Second Selection0  pindi nafasi za madarasa au shule mpya zitakapojengwa na kukamilika.

Kutokana na hali hiyo alitoa wito kwa wazazi kuwa wanapaswa kujitokeza kuchangia na kujenga vyumba vya madarasa haraka iwezekanavyo ambapo alihitaja Halmashauri ya Jiji la mbeya kuwa ndiyo wilaya yenye mzigo mkubwa kwa mahitaji ya vyumba 63 na wanafunzi 2660 hawajapata nafasi.

Alisema wanafunzi 86,568 waliandikishwa darasa la kwanza mwaka 2005 lakini waliofikia darasa la saba na kusajiliwa kwa ajili ya kufanya mtihani walikuwa 82,272 lakini wanafunzi 78,667 ndiyo walifanya mtihani huo wa darasa la saba mwaka 2011.

Lakini kati ya hao wanafunzi 259 walituhumiwa kuhusika na udanganyifu na baada ya uchunguzi wanafunzi 215 wamefutiwa matokeo baada ya kubainika na udanganyifu huo na 43, 440 walifaulu mtihani huo ambapo wasichana ni 22, 104 na wavulana ni 21,136

Aliitaj wilaya ambayo haukufaulisha sana kuwa ni wilaya ya Ileje ikifuatiwa na wilaya ya Mbozi ambapo mwanafunzi aliyeongoza kimkoa ni mwanafunzi kutoka shule maalum ya Uwata kutoka Jiji la Mbeya na kuwataja wanafunzi walioongoza kuwa ni John Mwaipopo kutoka shule ya Uwata na Vailet Sanga kutoka shule ya Msingi Airport.

Aidha alisema kuwa mbali na kujivunia na ufaulu huo wanafunzi saba walipata alama sifuri na kwamba shule kumi bora zimetoka wilaya ya Rungwe, Mbarali, Mbozi, na Jiji la Mbeya. 

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa baadhi ya walimu wa shule za sekondari za Serikali mkoani hapa wanawachangisha wazazi Shilingi 30,000 kwa ajili ya madawati na Shilingi 30,000 kwa ajili ya majengo hali inayowasababisha baadhi ya wazazi wenye uwezo mdogo kushindwa kuwapeleka wanafunzi wao kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger