Pages


Home » » UCHACHE WA VITENDEA KAZI WAKWAMISHA UZOAJI WA TAKA KATIKA MADAMPO MKOANI MBEYA

UCHACHE WA VITENDEA KAZI WAKWAMISHA UZOAJI WA TAKA KATIKA MADAMPO MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:35 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Uchache wa vitendea kazi vya kuzoa na kubeba taka umechangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha jitihada za uongozi wa jiji kuondoa taka kwenye madampo hali inayopelea dampo moja kukaa na taka kwa zaidi ya wiki moja.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa mtaa Rungwe kata ya Rwanda jijini Mbeya Baraka Mwakabula kupitia mahojiano na mwandishi wetu kuhusu hatua wanazokabiliana nazo ili kuondoa kero ya kujaa kwa taka katika madampo kwa zaidi ya wiki moja.

Amesema uchache wa magari ya kuzolea taka ni moja ya sababu kubwa iliyochangia kukwamisha zoezi la uzoaji taka na kuongeza kuwa kata ya Ruanda inatumia gari moja kwa zoa taka katika mitaa 4 ambayo ni mwanjelwa, soko la benki, soko la wa kulima  na soko la kabwe.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger