Pages


Home » » MDAHALO WA KATIBA MPYA TUNDUMA - MBOZI

MDAHALO WA KATIBA MPYA TUNDUMA - MBOZI

Kamanga na Matukio | 06:31 | 0 comments
Habari na chanzo maalum.
Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka amesema kuwa katika katiba mpya inayotarajiwa kuandikwa ni muhimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asiwe anakopa mikopo nje ya nchi bila kupitishwa na Bunge.

Ameyasema hayo katika mdahalo wa mchakato wa kuelekea kuandika katiba mpya na Tanzania tunayoitaka uliokuwa umeandaliwa na Muungano wa asasi zisizokuwa za Kiserikali wilayani Mbozi kwa kushirikiana na The foundation for Civil Society.

Aidha amesema katiba iyo pia iwazuie mawaziri kuingia mikataba pasipo Bunge kuridhia na kupitia mikataba hiyo ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza na kuziba mianya ya ufisadi.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mdahalo huo wamesema hakuna sabuba ya kuwepo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi katika wilaya moja na badala yake wamependekeza kuwepo kwa cheo kitakachosimamia wilaya

Akitoa sababu ya mdahalo huo Mwenyekiti wa asasi zisizo za kiserikali wilayani Mbozi Pilika Fumbo amesema kuwa mdahalo huo umelenga kuwaandaa wananchi kushiriki kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger