Pages


Hatarini kukubwa na Ugonjwa wa mlipuko kutokana na hali mbaya ya vyoo.

Kamanga na Matukio | 02:43 | 0 comments
 
Wanafunzi wa shule ya msingi Nero Jijini Mbeya wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na hali ya vyoo wanavyotumia.

 Hayo wameyasema hii leo wakati walipokua wakizungumza na mwandishi wetu wamesema hali ya vyoo shuleni hapo ni mbaya kutokana na  kujaa kwa takribani miezi saba hali inayowafanya kujisaidia vichakani na wengine kujisaidia pembeni ya tundu la choo.

 Mmoja wa wanafunzi hao Memori Kiandu amesema wamekuwa wakisumbuliwa na hali hiyo licha ya kuchangia shilingi elfu tatu kwa ajili ya kujengewa vyoo vingine.

 Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Gasper Lyimo  amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema mamlaka husika isimamie suala hilo  kwani limedumu kwa muda mrefu.

 Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Iyela Two Pipingu Mwakilasa amesema wameanza kujenga vyoo vingine kutokana na kujaribu kuzibua vyoo hivyo na kushindikana.

Kamati ya uchaguzi ya TFF imeendelea imetoa taarifa ya kurekebisha orodha ya pingamizi iliyotolewa katika vyombo vya habari.

Kamanga na Matukio | 02:42 | 0 comments

Na Shaban Kondo,

Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF imeendelea imetoa taarifa ya kurekebisha orodha ya pingamizi iliyotolewa katika vyombo vya habari kwa kueleza iliacha pingamizi lililowekwa na Paul Mhangwa dhidi ya Mugisha Galibona na Vedastus Lufano ambao wanaomba nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kupitia kanda ya pili (Mwanza na Mara).

Kamati ya uchaguzi ya TFF iomeomba radhi kwa pingamizi hilo kuachwa kwenye orodha iliyotolewa hapo jana katika vyombo vya habari, hivyo imesisitiza wahusika hao kufika bila kukosa katika kiksoi cha kujadili pingamizi kitakachofanyika jumatano Januari 30 katika ofisi za TFF kuanzia saa nne asubihi.

Katika hatua nyingine kamati ya uchaguzi ya TFF imewataka walioweka pingamizi dhidi ya wagombea nafasi mbali mbali za uongozi wa TFF kuwa na ustahamilivu katika kipindi hiki kwa ajili ya kuiachia kamati hiyo kufanya kazi yake ipasavyo.

Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo katibu mkuu wa TFF Angetille Osiah amesema hairuhusiwi kwa yoyote alioweka pingamizi dhidi ya wagombea kwenda katika vyombo vya habari na kuliweka wazi pingamizi lake.

Chama cha wendesha bajaji mkoani Mbeya kimetoa misaada mbalimbali katika kituo cha kulea watoto yatima.

Kamanga na Matukio | 02:42 | 0 comments

Mwenyekiti wa umoja Bajaji Mbeya Bw.Idd Ramadhan 
Chanzo:- Bomba FM 104.0MHz 
Chama cha wendesha bajaji  mkoani Mbeya kimetoa misaada mbalimbali katika  kituo  cha kulea watoto yatima  cha malezi na huruma kilichopo katika eneo la simike kwa lengo la kurudisha shukrani kwa wateja wake

Akizungumza na bomba fm mwenyekiti wa chama hicho  Idd Ramadhani amesema wamejiwekea mfumo wao kama chama cha bajaji kwa kufuata nyayo za mlenzi wa chama hicho Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo ili kuweza kuwasaidia wasiojiweza na kwamba kila wanajamii anapaswa kuguswa na kujitokeza kutoa misaada .  

Kwa upande wake katibu wa bajaji Ernest Mwaisangu  ameseviasa vikundi mbalimbali kuweza kujipanga na kuweza kutoa misaada kwa wasiojiweza  kuifahamisha serikali mambo muhimu ambayo yanafanyika katika kuisaidia jamii .

Kwa upande  Frank Musa mmoja wa  watoto hao  ametoa shkrani kwa chama hicho na kuwaomba kutokukata tama kuwasaidia ili nao waweze kuwasaidia wengine walitoa shukwani.

Aidha, kituo cha hicho kupitia mmoja wa walezi, kimetoa shukrani zake za dhati kwa umoja wa waendesha bajaji kwa kitendo cha kuwapatia misaada mbalimbali kituoni hapo.

Hata hivyo mdau mkuu wa umoja wa  wandesha bajaji hao Noah Mwakisu  vikundi vingine ili kuwapa hamasa zaidi na amevitaka vikundi vingine kuiga mfano kama huu waliouonyesha umoja wa bajaji  kwa kutoa misaada katika jamii

SHITAMBALA KUONGOZA MAANDAMANO WANANCHI 5000 KUMVAA KANDORO KUPINGA KUHAMISHWA

Kamanga na Matukio | 02:41 | 0 comments

MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa  Bw.Sambwee Sitambala

Asema  yatakuwa ya amani bila  Vurugu
Asema  sera ya  CCM ni kutetea  wananchi
MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa  Bw.Sambwee Sitambala  anatarajiwa kuongoza  maandamano  ya amani  ya wananchi  zaidi ya  5000 wa  mtaa  wa Gombe  kusini  kwenda  kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kupinga amri ya kutaka  kuwahamisha  kwenye  nyumba zao na eneo hilo kupewa  watu wengine.


Akizungumza   na waandishi wa habari baada ya kwisha  kwa mkutano wa wananchi hao diwani wa Kata ya  Itezi  jijini Mbeya  Bw.Frank Mayemba ambaye  pia ni mjumbe wa Mkutano  mkuu Taifa  CCM alisema kuwa  katika  maandamano hayo  watashirikiana  na  Bw.Shitambala  kuongoza   hadi kufika kwa mkuu wa Mkoa.


Alisema kuwa wananchi hao ambao zaidi ya asilimia  90 ni wanachama wa CCM walifikia  hatua hiyo baada ya kuona  hawasikilizwi  katika kilio chao ambacho wamekuwa wakitoa kwa Jiji la Mbeya kuwataka kutowagusa kwa kuwa walipewa maeneo hao kihalali baada ya kubadilishwa  matumizi yake  ya awali ambayo yalikuwa viwanda.
Bw.Mayemba alisema kuwa  kutokana na hali hiyo wamedhamiria  kudai haki yao kwa mkuu wa Mkoa ambaye  ndiye msimamizi wa Halmashauri zote Mkoa wa Mbeya  ambapo kutokana na hekima  yake  walisema kuwa wana imani kuwa atawasaidia kuwasikiliza  ombi lao na kusitisha  zoezi hilo ambalo ni  athari kubwa kwa wananchi hao.
Alisema kuwa  wananchi hao baada ya kupewa viwanja hivyo  wamekaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka  20 na hivyo kisheria kuwa  wamiliki haklali wa  maeneo haio wasio takiwa kubughudhiwa  na hivyo kushangaa wakati wote wanapoambiwa kuwa watahamishwa na  maeneo yao kupewa  watu wengine.
"sisi tunasema    kama viongozi wa chama   hakika hatutakubali  suala  hili kwa kuwa ni wamiliki  halali wa eneo hili  na hivyo kama wanataka kugawa  basi tuweke mkataba ambao  watatugawia  sisi na wala si wengine  kama wanavyotaka kufanya  sasa  hawa  wataalam."alisema.
Naye  Bw.Shitambala ambaye pia  ni Kaptain wa jeshi mstaafu na mwanasheria  maarufu alisema kuwa  ataongoza  maandamano hayo ya amani hadi kwa mkuu wa Mkoa   na hakuna vurugu itakayotokea  kwa kuwa  CCM ni chama kinachohamasisha  amani na utulivu na  hivyo wao wataonesha  mfano.
Kada huyo wa CCM ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla   ya kumamia  chama hicho alisema kuwa wataomba vibali polisi kwa ajili ya kulinda maandamano  hayo na kamwe hawatachoma  barabara kama wanavyofanya  wengine  ambnapo watapata nafasi ya kumweleza  mkuu wa Mkoa   hoja  zao zinazopinga  kuondolewa katika  eneo hilo .
Alisema   yeye kama  mkazi aliyejenga  eneo hilo ni dhambi kubwa kuona  wananchi wenzake na yeye akiwemo wakinyanyaswa   na hivyo kupelekea  hasira kali kwa chama  hali ambayo alisema kuwa katika  mkutano mkuu wa chama  na  vikao mbali mbali wamekubaliana kupinga  hali hiyo  na kuwapa haki yao wanachama .

Kwa hisani ya Charles Mwakipesile Mbeya

Meya Jiji la Mbeya asema wana mikakati juu ya kulijenga jiji la Mbeya.

Kamanga na Matukio | 02:14 | 0 comments
 Meya wa Jiji la Mbeya  Athanasi Kapunga,

Chanzo Bomba FM, Mbeya.
Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga  amesema  kumekua na  tabia ya  kuwepo msongamano wa abiria katika vituo vya mabasi yaendayo mikoani visivyo rasmi hasa kituo kidogo cha magari eneo la Mwanjelwa.

Akizungumza na Bomba FM amesema kuwa halmashauri ya jiji  imejipanga kushughulikia suala hilo na wana mikakati juu ya kulijenga jiji la Mbeya.

Amesema halmashauri ya jiji la Mbeya imedhamiria kuzirekebisha barabara zote kwa kiwango cha lami ambapo kila mwaka halmashauri itakuwa ikijenga barabara zenye urefu wa kilometa 10.

Aidha amesema ili kukabiliana na msongamano wa magari kati kati ya Jiji Halmashauri imedhamiria ya kujenga vituo vya mabasi yaendayo wilayani mwanzoni mwa mji.

Kapunga  amekiri  kuwa utaratibu wa sasa wa mipango miji si mzuri na halmashauri hiyo imejipanga katika mipango hiyo  ikiwa na nia ya kuboresha barabara za mitaa ili kupunguza vituo vya mabasi visivyo rasmi.  

Hata hivyo amekemea vikali vitendo vya  madereva ambao wamekuwa wakitoka eneo la stendi kuu na kuifanya stendi eneo la Mwanjelwa ambalo si rasmi kwa mabasi yaendayo  mikoani.
 Wakati huohuo ametoa wito kwa taasisi za kibenki kuanza kuangalia namna ya kujenga ofisi zao pembezoni mwa mji ili kurahisisha huduma kwa wananchi wanaolazimka kuja mjini kuzifuata

Chama cha madereva bajaji mkoani Mbeya kimedhamiria kurejesha shukrani zake kwa wateja

Kamanga na Matukio | 02:13 | 0 comments


Mwenyekiti wa umoja Bajaji mbeya Bw.Idd Ramadhan  

Chama cha madereva bajaji mkoani Mbeya kimedhamiria kurejesha shukrani zake kwa wateja wake kwa makundi maalum kwa kutoa misaada mbalimbali

Mwenyekiti wa chama hicho Idi Ramadhan amesema kwa kuanza chama hicho kitawatembelea watoto yatima katika kituo cha Isalaga kilicho Uyole Mbeya na zoezi hilo litafanyika kila mwisho wa mwezi.

Wakati huohuo amewataka vijana kuungana kwa pamoja katika kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuondokana na tabia ya kukaa vijuweni huku wakilalamika tatizo la ajira.

Aidha ameiomba Serikali kutimiza dhamira yake ya kusaidia vijana kwa vitendo ili waweze kuondokana na vitendo vya uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya.

Chama cha wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza PFA, kimemkana winga kutoka nchini ubelgiji na klabu ya Chelsea Eden Hazard.

Kamanga na Matukio | 02:12 | 0 comments
Eden project: How Hazard will look in Chelsea blue 
 Eden Hazard
  Na Shaban Kondo.
 Chama cha wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza PFA, kimemkana winga kutoka nchini ubelgiji na klabu ya Chelsea Eden Hazard kufuatia sakata la kumpiga kijana anaeokota mipira katika uwanja wa Liberty Charlie Morgan wakati wa mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi uliochezwa usiku wa kuamkia jana.

Chama cha wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza PFA, kimemkana winga huyo kupitia kwa mtendaji wake mkuu Gordon Taylor ambapo amesema Eden Hazard hana mamlaka ya kujichukulia sheria mkononi, zaidi ya kuacha sheria zilizotungwa zichukue mkondo wake juu ya sakata la kumpiga kijana muokota mipira. 

Amesema tukio hilo moja kwa moja linajidhihirisha wazi kwamba chama cha soka nchini Uingereza kitamuadhibu mchezaji huyo kutokana na kile alichokitenda na wao kama chama cha wachezaji wa kulipwa hawawezi kuingilia kutokana na hali halisi kutohitaji utetezi.

Hata hivyo Gordon Taylor amesema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka FA kama itawafikia na endapo watahitajika kwa ajili ya kumtetea mchezaji huyo watajitokeza lakini wanaamini kisu cha sheria kitamkata Eden Hazard.

Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez amekiri mchezaji wake alifanya makosa makubwa ya kumpiga kijana huyo, lakini bado akaendelea kusisitiza kwamba bado suala hilo lina wigo mpana wa kujadiliwa.

Hata hivyo Benitez ameshauri suala hilo kutazamwa upya kutokana na kijana Charlie Morgan kuchangia kitendo alichofanyiwa kufuatia kitendo cha kuupiga mpira kabla ya kutaka kuukota, na hivyo kumsababishia Hazard kuamini huenda alikua anapoteza muda kwa makusudi.

Wakati huo huo Eden Hazard ameomba radhi kufautia kitendo cha kumpiga Charlie Morgan kwa kusema halikua kusudio lake kumpiga kijana huyo bali alitaka kuupiga mpira na kwa bahati mbaya alijikuta anafanya tofauti.

Amesema anajua jamii itayapokea maneno hayo tofauti lakini amesisitiza ukweli ndio huo na hana lingine la kusema zaidi ya kumtaka radhi Charlie Morgan pamoja na jamii ya soka ulimwenguni kote.

Baada ya kitendo hicho Eden Hazard alionyeshwa kadi nyekundu huku akiiacha timu yake ikiangamia kwa kutolewa kwenye michuano ya kombe la ligi dhidi ya Swansea ambao wametinga katika hatua ya fainali kwa jumla ya mabao mawili kwa sifuri waliyoyapata katika mchezo wa awali kabla ya usiku wa kuamkia jana ambapo waliambulia matokeo ya sare ya bila kufungana.

Wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzani bara wametangaza kuwa tayari kwa kipyenga cha mzunguko wa pili wa ligi hiyo'

Kamanga na Matukio | 02:10 | 0 comments
Na Shaban Kondo. Wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzani bara wametangaza kuwa tayari kwa kipyenga cha mzunguko wa pili wa ligi hiyo kitakachopulizwa kuanzia Januari 26 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Vodacom inayodhamini ligi kuu, Salum Mwalim amesema kwamba kampuni yake inajisikia fahari kuona soka sasa inachezwa viwanjani zaidi na si nje hivyo wanatarajia upinzani mkubwa katika mzunguuko wa pili.

Salum Mwalim pia akatoa shukurani kwa TFF pamoja na kwa kamati ya Ligi kufautia ushirikiano mzuri wanaowaonyesha, katika kuendeleza na kuleta chachu ya ligi kuu ya soka Tanzania bara ambayo mwanzoni mwa msimu huu ilianza kwa changamoto kadha wa kadha.

Wakati huo huo shirikisho la soka nchini TFF kupitai kwa Afisa habari Bonifas Wambura limetoa kauli ya kuwa tayari kwa kipyenga cha mzunguko wa pili, kupulizwa baada ya kukamilisha maandalizi yote yanayostahili.

Michezo ya ligi kuu itakayochezwa mwishoni mwa juma hili ni kati ya;


African Lyon
 - 
SIMBA Sports Club
Mtibwa Sugar
 - 
Police Morogoro
Coastal Union
 - 
Mgambo JKT
Ruvu Shooting
 - 
JKT Ruvu
Azam
 - 
Kagera Sugar
JKT Oljoro
 - 
Toto Africans


Wakati matayarisho ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu msimu huu yakiwa katika mstari wa mafanikio kwa mara ya kwanza wadhamini wa ligi hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya LAJANN E-SYSTEMS ENTERPRISE wamezindua tovuti maalum itakatohusika na ligi kuu. 

Daniel Mwakamele msemaji wa msemaji wa Kampuni ya LAJANN amesema wamefanikisha uzinduzi huo baada ya kufanya kazi kwa umakini huku wakiamini kila mtanzani watakua akipata taarifa za ligi kwa wakati na kwa umakini.

TBL yakabidhi vifaa vya Michezo kwa Klabu kongwe nchini Simba na Yanga,

Kamanga na Matukio | 02:10 | 0 comments
Na Shaban Kondo,
 Wadhamini wa klabu kongwe nchini Simba na Yanga, kampuni ya bia nchini TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro jana wamekabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa klabu hizo kwa ajili ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe amesema wanaamini klabu hizo kongwe zimejiandaa vyema na zipo tayari kwa mshike mshike wa ligi mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara unaoatarajiwa kuanza siku ya jumamosi.

Baada ya kupokea vifaa hivyo katibu mkuu wa klabu ay Dar es salaam young Africans Lawrence mwalusako amesema wamefarijika kupata vifaa hivyo ambapo hatua hiyo bado inaendelea kutamani kufanya kazi na kampuni ya bia nchini TBL kufuatia utaratibu wake wa kufanya kazi kwa kufuata mkataba unavyoelekea.

Kwa upande wa mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba ambao waliwakilishwa na msemaji wao Ezekiel Kamwaga katika hafla hiyo wameishukuru kampuni ya bia nchini TBL na wameahidi kufanya jitihada za kutetea ubingwa wao msimu hukua kikumbushia mazuri ambayo wamekua wakiyafanya katika miaka inayoishia na tatu.

Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini TFF imeahidi wadau wa mchezo huo itafanya kazi zake kwa misingi ya haki.

Kamanga na Matukio | 01:27 | 0 comments



Na Shaban Kondo,
 Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini TFF imeahidi wadau wa mchezo huo itafanya kazi zake kwa misingi ya haki katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mku wa TFF utakaofanyika jijini Dar es salaam Februari 24.

Mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa baada ya waraka wa mabadiliko ya katiba ya TFF kupitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu mwishoni mwa mwaka jana Idd Mtiginjola amesema kamati yake itasimamia misingi ya haki kwa kuvitafsiri vifungu vya katiba pamoja na kanuni za uchaguzi endapo rufaa iltawasilishwa kwao.

Awali katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Angetille Osiah aliitambulisha kamati hiyo ya rufaa kwa waandishi wa habari na kutoa sababu za kuundwa kwa kamati hiyo itakua ikifanya kazi zake kwa mara ya kwanza baada ya kuingizwa katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu.

Amesema sababu za kuundwa kwa kamati hiyo ni kutaka kutanua wigo wa kupatikana kwa haki pale litakapojitokeza masuala ya utata kama ilivyokua siku za nyumba ambapo kamati ya uchaguzi ilikua inajibebesha majukumu ambayo yalikua si halali kwake.

Baada ya utambulisho huo Angetille Osiah aliwakabidhi wajumbe wa kamati hiyo vitendea kazi  mbalimbali zikiwemo kanuni za uchaguzi za TFF na wanachama wake, Katiba ya TFF na Katiba ya Shirikisho la soka la Kimataifa la (FIFA).

Mbali ya Iddi Mtiginjola, wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Makamu Mwenyekiti, Francis Kabwe ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama Rufani ya Tanzania, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria.

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.

TUKIWA BADO KATIKA UCHAGUZI WA TFF.

Kamanga na Matukio | 01:26 | 0 comments
Bwana Fredrick Mwakalebela aliekua Katibu Mkuu wa TFF
 Aliekua katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Fredrick Mwakalebela amezungumzia uchaguzi wa shirikisho hilo kwa kuitazama nafasi ya uraisi inayoonekana kutoa upinzani kwa Jamali Malinzi pamoja na Athumani Nyamlani ambae kwa sasa ni makamu wa kwanza wa raisi.

Mwakalebela ambae alitenda kazi zake kwa uadilifu mkubwa akiwa TFF kabla ya kutangaza kuaiacha nafasi ya ukatibu na kuingia katika masuala ya kisisa mwaka 2010, amesema licha ya kuwepo kwa mgombea  Omary Mussa Nkwarulo katika nafasi ya uraisi, bado anaona upinzani mkubwa bado upo kwa Jamali malinzi pamoja na Athumani Nyamlani.
 
Hata hivyo Fredrick Mwakalebeka akawataka wajumbe wa TFF kutumia nafasi yao ya kupiga kura kwa uadilifu mkubwa kutokana na hitaji la soka la bongo ambalo kwa sasa lina hamu ya kupata mafanikio kama ilivyo kwa nchi nyingi barani Afrika na kwingineko.


Wakati huo huo Uongozi wa chama chama cha makocha wa soka TAFCA mkoa wa umeyapokea kwa mikono miwili maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya TFF ya kuuahirisha uchaguzi wa chama hicho taifa uliokua umepangwa kufanyika JAnuari 19 jijini Dar es salaa.

Katibu mkuu wa TAFCA Abubakari saidi Behengula amesema pamoja na maamuzi hayo kuchelewa kutplewa kwa wakati bado anaamini TAFCA itapata nafasi ya kujipanga upya na kufuata taratibu za kikatiba kwa ajili ya kukamilisha uchaguzi mkuu ambao umeamishwa kufanyika baada ya uchaguzi wa TFF.

Hata hivyo Saidi Behengula akaendelea kuzungumzia jambo linguine ambalo kwa upande wa Mwanza wameliona ni la busara zaidi baada ya kuutumia mkutano wa uchaguzi wa TAFCA kuwa kama mkutano mkuu wa kujadili agenda mbali mbali.

Amesema suala kubwa lillilomfurahisha ni kukubaliana kwa pamoja kuwa uongozi wa TAFCA taifa uliopo madarakani kupewa ridhaa ya kuendelea na kufuta kasumba ya kuunda kamati ya muda ya uongozi.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limelitoza faini ya dola 10,000 Shirikisho la Soka la Ethiopia .

Kamanga na Matukio | 01:25 | 0 comments

AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZE

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limelitoza faini ya dola 10,000 Shirikisho la Soka la Ethiopia baada ya mashabiki wake kutupa mavuvuzela pamoja na chupa za maji uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Zambia ambao walitoka sare ya bao 1-1 Jumatatu.

CAF ilitangaza kuwa nusu ya adhabu hiyo ya dola 10,000 itasamehewa kama tu mashabiki wa Ethiopia hawatarudia tukio hilo katika kipindi chote cha mashindano.

Ethiopia inayoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon kwa mara ya kwanza baada ya miaka 31 ina mashabiki wengi waliokuja kuiunga mkono timu yao lakini mchezo wao wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Mbombela uliingia dosari baada ya mwamuzi Eric Otogo-Castane alipompa kadi nyekundu golikipa Jemal Tassew muda mchache kabla ya mapumziko.

Mara baada ya mwamuzi huyo kutoa kadi vuvuzela na chupa za maji zilimiminika uwanjani zikitokea jukwaani huku makocha na wachezaji wa akiba wakijificha wasiumizwe na vitu hivyo wakati mtangazaji uwanjani hapo alikiwaomba mashabiki hao kutulia.

Mashabiki hao wa Ethiopia pia wanaweza kufungiwa kuingia uwanjani katika mchezo wa Ijumaa dhidi ya Burkina Faso labda CAF ipate uhakika kutoka EFF kuwa watawadhibiti mashabiki wao.

 Wakati huo huo WENYEJI wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, Afrika Kusini, maarufu kama Bafana Bafana, leo wamefanikiwa kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia Robo Fainali baada ya kuichapa Angola Bao 2-0 katika Mechi ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Moses Mabhida huko Jijini Durban.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Bafana Bafana baada ya kutoka sare na Cape Verde katika Mechi ya ufunguzi.

+++++++++++++++

MAGOLI:

South Africa 2

-Siyabonga Sangweni Dakika ya 30

-Lehlohonolo Majoro 62

Angola 0

+++++++++++++++

Aliewapa Bafana Bafana Bao lao la kwanza ni Senta hafu Siyabonga Sangweni katika Kipindi cha Kwanza na Lehlohonolo Majoro kupiga la pili Kipindi cha Pili.

Baadae leo itakuwepo Mechi ya pili ya Kundi A kati ya Morocco na Cape Verde ambayo pia itachezwa Uwanja wa Moses Mabhida huko Mjini Durban.

VIKOSI:

South Africa: Khune, Ngcongca, Khumalo, Sangweni, Masilela, Mahlangu, Furman, Phala, Parker, Mphela, Rantie

Akiba: Sandilands, Gaxa, Nthethe, Majoro, Tshabalala, Serero, Matlaba, Letsholonyane, Manyisa, Meyiwa.

Angola: Lama, Airosa, Dany Massunguna, Miguel, Bastos, Pirolito, Mateus, Dede, Geraldo, Guilherme, Manucho

Akiba: Landu, Lunguinha, Fabricio, Djalma, Manucho Dias, Zuela, Gilberto, Amaro, Yano, Mingo Bile, Manuel, Neblu.

Refa: Koman Coulibaly (Mali)

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger