Pages


MKURUGENZI WA JIJI ASEMA BARABARA IMETENGEWA MILIONI 400 KWA AJILI YA UKARABATI.

Kamanga na Matukio | 07:02 | 0 comments
UFAFANUZI:- Ukarabati wa barabara wa aina yake tofauti na utaalamu yakinifu, Mkurugenzi wa Jiji Bwana Juma Idd amesema hatua hii ni ya muda kwani barabara hiyo imetengewa jumla ya shilingi milioni 400, ambapo Mkandarasi amekwisha patikana na shughuli za ukarabati zitaanza mara baada ya msimu wa mvua kuisha. 

 Mtandao huu umeshuhudia ukarabati ukiendelea eneo la Kanisa la Sabato barabara ya Mbalizi kutokea Meta jijini hapa ambapo Saruji imetumika kuziba viraka katika barabara hiyo, badala ya kutumia Lami ambapo huigharimu serikali kutokana na viraka hivyo kubanduka baada ya muda mfupi. 

Hata hivyo mwaka uliopita barabara hiyo iligharimu shilingi milioni 57, licha ya Mkurugenzi huyo kutokuwa tarai kutaja kiasi cha gharama zilizotumika kukarabati barabara hiyo kwa mwaka huu na kudai kuwa ni kiasi kidogo kimetumika.

Wakati huo huo Baraza la madiwani wa Kata zote 36 za jiji la Mbeya limelalamika kuwepo kwa miundombinu mibovu ya barabara hizo na utendaji mbovu wa makandarasi ambao huzijenga barabara hizo licha ya kupewa pesa nyingi.

NMB MBEYA YATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IKUTI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:53 | 0 comments
Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa misaada ya maguni 112 ya mahindi, maharage magunia 23 na mafuta ya alizeti lita mia tatu, kwa waathirika wa mafuriko wa mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga jijini Mbeya.

Akikabidhi msaada hauo Meneja wa Benki hiyo Bwana Nazareth Lebi, mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama na Mbunge wa Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi, amesema msaada huo umegharimu shilingi milioni 10 za kitanzania na kwamba benki yake inawathamini na kuwajali wateja wake.

Ameongeza kuwa benki hiyo inashirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali yakiwemo majanga, elimu na michezo kwani fedha zinazotolewa ni sehemu ya faida wanayoipata, hivyo wanawarudishia wananchi katika matukio mbalimbali na wananchi wa Ikuti ni sehemu ya wateja wao.

Bwana Nazareth amezitaka asasi nyingine ziendelee kutoa msaada kwa wananchi hao kwani athari yake ni kubwa hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kutokana na kipindi hiki kigumu kutokana na wananchi hao kushindwa kulima na kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi kutokana na baadhi yao kukosa sehemu za kuishi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Bwana Evansi Balama akipokea msaada huo ameishukuru benki hiyo kwa moyo wa uzalendo wa kuwajali wateja wake.

Naye Mbunge wa jimbo la Mbeaya Mjini Bwana Joseph Mbilinyi ameishukuru benki ya NMB kwa kuwathamini wananchi na kujali janga la mafuriko ambalo huathiri kwa kwa kiasi kikubwa shughuli za kimaendeleo.

WATU WAWILI JINSI YA KIUME WAMEUAWA KWA UJAMBAZI - RUNGWE, MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:35 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe.
Watu wawili jinsi ya kiume wamekutwa wameuawa na wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Kinyika, kata ya Ikuti wilaya ya Rungwe wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya wizi.

Watu hao wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya marehemu kufanikiwa kuvunja kisha kuiba vitu mbalimbali vya thamani kwenye nyumba ya bwana Zakayo Ngela ambapo mara baada ya marehemu hao kutenda tukio hilo bwana Zakayo alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa wananchi ambao walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa hai.

Hata hivyo uhai wa watuhumiwa hao ulikatishwa na wananchi wenye hasira kali ambao walikuwa wakiwashambulia wezi hao kwa kutumia vitu mbalimbali vigumu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa upelelezi zaidi unaendelea wa tukio hilo na kuwataka wananchi kuwafikisha watuhumiwa kwenye vituo vya polisi badala ya kujichukulia sheria mkononi.

MDAHALO WA KATIBA MPYA TUNDUMA - MBOZI

Kamanga na Matukio | 06:31 | 0 comments
Habari na chanzo maalum.
Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka amesema kuwa katika katiba mpya inayotarajiwa kuandikwa ni muhimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asiwe anakopa mikopo nje ya nchi bila kupitishwa na Bunge.

Ameyasema hayo katika mdahalo wa mchakato wa kuelekea kuandika katiba mpya na Tanzania tunayoitaka uliokuwa umeandaliwa na Muungano wa asasi zisizokuwa za Kiserikali wilayani Mbozi kwa kushirikiana na The foundation for Civil Society.

Aidha amesema katiba iyo pia iwazuie mawaziri kuingia mikataba pasipo Bunge kuridhia na kupitia mikataba hiyo ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza na kuziba mianya ya ufisadi.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mdahalo huo wamesema hakuna sabuba ya kuwepo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi katika wilaya moja na badala yake wamependekeza kuwepo kwa cheo kitakachosimamia wilaya

Akitoa sababu ya mdahalo huo Mwenyekiti wa asasi zisizo za kiserikali wilayani Mbozi Pilika Fumbo amesema kuwa mdahalo huo umelenga kuwaandaa wananchi kushiriki kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.

MUJATA - JESHI LA POLISI HALIWEZI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU BILA KUSHIRIKIANA NA JAMII

Kamanga na Matukio | 06:27 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu
Chama cha Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kimesema kuwa Amani na utulivu kamwe haiwezi kudumishwa na jeshi la polisi pekee bali ni kwa ushirikiano kutoka kwa jamii.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa MUJATA Chifu Shayo Soja wakati wa mahojiano ofisini kwake na kuongeza kuwa jeshi la polisi halina budi kusimamia nidhamu ya askari wake ambao wamekuwa wakitenda kazi zao bila kufuata misingi ya jeshi hilo.

Aidha ametoa ushauri kwa jeshi la polisi kuunda Sera moja ya ulinzi itakayotumika Tanzania bara na visiwani ambayo pia itafikishwa kwa wananchi na kuwaeleza umuhimu wa wao kushiriki katika ulinzi.

Wakati huohuo amevita vyama vya siasa kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya kidemokrasia badala ya kutumia mwanya huo wa demokrasia kusababisha vurugu na kujenga matabaka hapa nchini.

WANANCHI WAFICHUA TUHUMA KWA JESHI LA POLISI KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UNYANYASAJI NA RUSHWA - MBOZI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:24 | 0 comments
Habari na chanzo chetu.
Wananchi wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wamelipua lawama jeshi la polisi wilayani humo kwa kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji na kupokea rushwa kutoka kwa wananchi.
Lawama hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti kupitia barua za malalamiko ambazo zimeandikwa na wananchi na kufikishwa ofisi ya haki za binadamu.
Katika barua hizo wananchi wamelilalamikia jeshi hilo kwa kubambikizia wananchi kesi, baadhi ya viongozi wa vituo vya polisi kutishia kuuwa raia wanapofatilia haki zao na kushiriki kuwanyima haki wakulima pindi wanapokuwa kwenye migogoro na matajiri.
Aidha wananchi hao wamemuomba kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi kuwachukulia hatua za kisheria askari wake ambao wamekuwa wakitumia nafasi ya uaskari kunyanyasa raia.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi ameahidi kufuatilia malalamiko hayo na kuwataka wananchi kufikisha malalamiko kwenye ofisini yake badala kufikisha taarifa kwa watu ambao hawataweza kudhibiri tabia hizo

SARUJI YATUMIKA KUKARABATI BAADHI YA BARABARA YA LAMI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:55 | 0 comments
Ukarabati wa barabara wa aina yake tofauti na utaalamu yakinifu, mtandao huu umeshuhudia ukarabati ukiendelea eneo la Kanisa la Sabato barabara ya Mbalizi kutokea Meta jijini hapa ambapo Saruji imetumika kuziba viraka katika barabara hiyo, badala ya kutumia Lami ambapo huigharimu serikali kutokana na viraka hivyo kubanduka baada ya muda mfupi. 
Hata hivyo viongozi wa kitaifa wamekuwa hawapitishwi katika barabara hiyo kwa hofu ya kugundua ubadhilifu huo kutokana na kila mwaka barabara hiyo kukarabatiwa na Halmashauri ya jiji kwa kutumia makandarasi tofauti tofauti.


UFUNDI STADI:- BINTI MDOGO AJIHUSISHA NA UTENGEZAJI WA PIKIPIKI GEREJINI.

Kamanga na Matukio | 06:45 | 0 comments
Binti huyo pichani Happy Pius (9) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano ni mtoto mwenye kipaji cha pekee na kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kwa umahiri anaounesha kwa kutengeneza Pikipiki . Pichani Binti huyo akirekebisha moja ya Pikipiki kubwa aina ya Toyo Cruiser inayomilikiwa na kampuni ya vinywaji ya Cocacola iliyoletwa katika Gereji iliyopo eneo la Srereo Jijini Mbeya kama alivyokutwa na mpigapicha wetu jana.(Picha na Ezekiel Kamanga) 
Binti huyo pichani Happy Pius (9) akirekebisha moja ya Pikipiki aina ya Honda 250 iliyoletwa katika Gereji iliyopo eneo la Srereo Jijini Mbeya kama alivyokutwa na mpigapicha wetu jana.(Picha na Ezekiel Kamanga) 

UHABA WA MAFUTA MBEYA BAADHI YA WATEJA WAGOMEWA KUUZIWA MAFUTA HAYO.

Kamanga na Matukio | 06:36 | 0 comments
 Baadhi ya wateja wa mafuta wakiwa katika foleni katika kituo cha mafuta cha GAPCO kilichopo eneo la Mafiati jijini Mbeya kutokana na uhaba wa mafuta, hali iliyopelekea kuathiri shughuli mbalimbali za uzalishaji na usafirishaji kusimama na kupanda bei.
Dereva na Kondakta wa gari ya abiria maarufu daladala wakijadiliana jambo baada ya kugomewa kuuziwa mafuta pasipokuwa na sababu maalumu ambapo mtandao huu ulibaini kuwepo na ubaguzi katika uuzaji wa mafuta kutokana na kuangaliwa makampuni na umuhimu wa uhitaji kwa mteja.
*****
Habari na Mtandao huu.
Wamiliki wa vituo vya mafuta jijini Mbeya wameanza mgomo wa kuuza mafuta kuanzia jana majira ya saa tatu za usiku ambapo kituo kimoja cha BP ndicho kilichoonekana kuendelea kuuza mafuta jijini hapa.

Vituo hivyo vimefikia hatua ya kugoma kutoa huduma ya mafuta kwa jamii tangu mamlaka ya udhibiti wa nishati na madini (EWURA) itangaze kushusha bei ya mafuta aina ya Petroli kutoka shilingi elfu mbili mia moja kwa lita hadi kufikia shilingi elfu moja mia tisa themanini na tisa kwa sasa.

Kwa upande wake afisa habari wa EWURA bwana Taitus Kaguo amesema tatizo la mafuta kwa mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini inatokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara eneo la kitonga ambayo inasababisha magari ya mizigo kushindwa kupita.

Wakati huohuo amesema katika kukabiliana na tatizo la migomo kwa miliki wa vituo vya mafuta kuanzia mwakani bei ya mafuta itakuwa ikipanda na kushukwa kila baada ya mwezi.

Naye meneja wa mamlaka ya usafiri wan chi kavu na maji SUMATRA mkoa wa Mbeya Amani Shamaje amewataka abiria kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo nauli itapandishwa kutokana na kuwepo wka malalamiko kutoka kwa baadhi ya abiria kuwa nauli kutoka Mwanjelwa hadi Mbalizi kupanda kutoka shilingi mia tatu hamsini ya kawaida hadi kufikia shilingi mia tano.

BENKI KUU YA DAMU NYANDA ZA JUU KUSINI INAKABILIWA NA UHABA WA DAMU SALAMA.

Kamanga na Matukio | 06:21 | 0 comments
Picha ni mmoja wa wanafunzi walioguswa na zoezi la uchangiaji wa damu salama, kutokana na Benki ya damu ya nyanza za juu kusini kukabiliwa na upungufu mkubwa wa damu.
*****
Habari na mtandao huu.
Benki ya damu kanda ya nyanda za juu kusini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali ambayo inahatarisha usalama wa maisha hasa kwa akina mama wajawazito na wagonjwa wanatoakanao na ajali ambao wamekuwa wakihitaji damu kwa wingi.

Akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake meneja wa benki kuu ya kuchangia damu kanda ya nyanda za juu kusini dokta Baliyima Lelo amesema kuwa benki hiyo inaupungufu wa chupa mia moja za damu salama.

Amesema benki hiyo huitaji chupa mia tatu kila siku za damu salama lakini kwa sasa benki hiyo ambayo husambaza damu katika hospitali zote za mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini imekuwa ikipata lita 200 za damu salama badala ya mia tatu.

Kutokana na tatizo hilo Dokta Lelo ameiomba jamii kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha kwa wagonjwa wenye uhitaji mkubwa wa damu hasa kwa akina mama wajawazito ambao mara nyingi wamekuwa wakionekana kuwa na upungufu wa damu mwilini.

KANISA KATOLIKI JIMBO LA MBEYA LAINGIA DOSARI

Kamanga na Matukio | 06:15 | 0 comments
Habari na Mtandao huu
Kanisa katoliki jimbo la Mbeya limeingia dosari baada ya Padri Inosent Sanga anayesimamia masuala ya elimu ya jimbo hilo kuwafukuza bila kulipa stahiki zao baadhi ya waalimu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Fransisko.

Licha ya padri Sanga kushindwa kuwa na ustahimilivu kwa watumishi wake hao pia alikaidi agizo la mahakama ambayo iliagiza watumishi hao kuendelea kuishi kwenye nyumba zinazomilikiwa na kanisa katoliki hadi hapo watakapo lipwa madai yao bada ya kufukuzwa kazi.

Waalimu hao waliondolewa vyombo vya nje na kampuni ya Yono Auction Mart and Cout Broker tawi la Mbeya amapo hata hivyo vyombo vya waalimu hao vilirudishwa ndani kwa nguvu na Serikali ya wilaya baada ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Evansi Balama kufika eneo la tukio na kuzungumza na pande zote mbili.

Hata hivyo msemaji huyo wa shule ya senti frasisko padri Inosent Sanga aligoma kuzungumza lolote kwa waandishi wa habari.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa kitendo kilichofanywa na padri huyo si cha kiungwana na kwamba hakiendani na maadili ya mwenyezi Mungu.

MISAADA YAENDELEA KUTOLEWA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 06:13 | 0 comments
Mvua kumbwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi na msaada wa haraka wa vyakula na madawa unahitajika ili kuweza kunusuru maafa. Mbali na nyumba kubomoka mvua hiyo iliyodumu kwa muda wa masaa mawili imeweza kuharibu mimea ya mazao shambani. miundombinu ua Maji, Umeme na Barabara kutokana na mafuriko.
Vitongoji vilivyoathiriwa na mvua hiyo katika kata hiyo ni pamoja na kitongoji cha Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 *****
 Habari na Mtandao huu.
Wakazi wa kata ya Ikuti jijini Mbeya waliokubwa na mafuriko disemba 19 mwaka huu wameendelea kupata misaada kutoka kwa wadau mbalimbali ambapo jana mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ameliwapatia msaada wa gunia 40 za mahindi.

Mbunge huyo alikabidhi msaada huo kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyunga, Adia Mwambela chini ya uangalizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Mbeya Ulimboka Mwakilili ambaye alikabidhiwa jukumu la kuwagawia chakula hicho

Mbunge huyo amesema mahindi hayo yametolewa na wakazi wa jiji la Mbeya ambao walihudhuria tamasha la uzinduzi wa albamu yake ya anti vailasi.

Katika tamasha hilo kiingilio kilikuwa ni shilingi elfu tatu na alikuwa ameahidi kutoa shilingi elfu moja katika kila tiketi ili kusaidia watu waliokubwa na mafuriko kata ya Ikuti na kwamba tamasha lake liliingiza shilingi milioni 3 na laki 6

Kwa upande wake afisa Mtendaji wa Kata ya Iyunga, Adia Mwambela alitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa kata ya Ikuti kwa chakula hicho na kuahidi kukifikisha kwa wahusika.
 
Wakati huo huo Benki ya NMB inatarajia kwenda kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZA ATHIRI MAKAZI NA MIUNDOMBINU MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:02 | 0 comments
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Juma Idd(kushoto), akizungumza na Diwani wa kata ya Uyole baada ya kata yao kukumbwa na mafuriko makubwa baada ya mvua iliyonyesha jana, kudumu kwa muda wa saa moja kuanzia majira ya saa kumi hadi za kumi na moja za jioni. 

Mafuriko hayo yamesababisha nyumba kadhaa kubomoka na baadhi ya wananchi kukosa hifadhi na kuathiri kambi ya Wachina waliopo jijini hapa kwa ajili ya ujenzi wa barabra ambapo baadhi ya magari yao nusura yabebwe na maji ya  mafuriko hayo.

HITIMISHO:- Hata hivyo imeelezwa chanzo cha mafuriko hayo kinatokana na miundombinu mibovu ambapo wakala wa Barabara TANROADS kushindwa kudhibiti hali hiyo kwa muda mrefu licha ya kusisitizwa kupanua na kurekebisha mifereji ya kupitishia maji kiurahisi, pia kilimo kinacholimwa katika eneo la Igawilo kimeendelea kufunga mifereji ya asili ya kupitishia maji.

Wakati huo huo wataalamu kutoka kitengo ya mipango miji, TANROADS, maafa jiji na wilaya ya Mbeya, wanatarajiwa kutembelea Kata hiyo ilikuweza kutathimini hasara zilizotokea hapo jana katika mafuriko hayo.

MJOMBA AMCHOMA NA KAA LA MOTO MPWA WAKE KIGANJANI KWA TUHUMA ZA KUKOSA ADABU.

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments


Mtoto Oscar Oliver (17), mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya akiwa ndani ya ofisi za Jeshi la Polisi zilizopo Kituo cha Kati Mbeya, baada ya kuchomwa kiganja cha mkono wake wa kushoto na kaa la moto na mjomba wake kwa kile kinachodaiwa kuwa mtoto huyo kakosa adabu.


Mjomba wa mtoto Oscar Oliver, akiwa tayari kutiwa mikononi mwa Polisi baada ya kubainika kumuunguza kiganja cha mkono wa kushoto mtoto huyo kwa madai kakosa adabu.


 *****
Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya
Mtoto Oscar Oliver (17) mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya amechomwa na kaa la moto kiganja cha mkono wa kushoto na mjomba wake kwa tuhuma za kukosa adabu.

Tukio hilo la kinyama limetokea usiku wa kuamkia siku ya sikukuu ya Kristmas nyumbani kwa Andendekisye Mwakabubu (30) ambaye ndiye anayedaiwa kufanya unyama huo kwa mpwa wake akimtuhumu kuwa alitaka kumwibia.

Mwakabubu anadaiwa kumlazimisha mtoto huyo kushika kaa la moto na baada ya mtoto huyo kuungua kiganja chake alimpeleka katika kituo kidogo cha polisi cha Mwanjelwa na kumfunmgulia kesi ya wizi wa kuibiwa vitu mbalimbali ili kuweza kuficha unyama wake huo.

Baada ya kufungua kesi hiyo, askari polisi walimshikilia kijana huyo na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi mkoani hapa na kumweleza mlalamikaji huyo bandia kuwa alitakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mtoto huyo kupelekwa mahakamani.

Mtoto huyo alipofikishwa katika kituo hicho kikuu alikutana na askari waliopo ndani ya kitengo cha kuelimisha jamii kuhusu unyanyasaji wa kijinsi hususani kwa watoto ambao walimsikiliza mtoto huyo na hatimaye jana walimwita mpwa wake kwa ajili ya kutoa maelezo.

Mwakabubu baada ya kufika kituoni hapo na kutoa maelezo na kuulizwa kuwa nani aliyehusika na tukio hilo alishindwa kubainisha huku akisema kuwa hajui aliyemchoma huku akisahau kuwa katika maelezo yake ya awali yeye ndiye alikuwa mlalamikaji jambo ambalo liliwashawishi askari hao kumakamata na kumpeleka rumande.

Mpwa huyo wa mtoto Oscar akiwa mahabausu ya kituo hicho cha polisi, askari hao wanaunda mtandao huo wa kuelimisha jamii juu ya unyanyasaji wa kijinsia mkoani hapa hususani kwa watoto walimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Mwakabubu alihojiwa na askari wa mtandao huo wakiongozwa na askari aliyefahamika kwa jina la Pudensiana Baito huku mwandishi wa habari hizi akiwa anafuatilia tukio hilo na askari huyo alipotakiwa kueleza kwa undani tukio hilo alisema kuwa yeye si msemaji wa jeshi la polisi.

PADRI AWATIMUA WALIMU 7 KAZINI NA KUWATUPIA VYOMBO VYAO NJE, BILA KUJALI MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments
Padri Mbeya atimua walimu
      Walala nje siku mbili
*       DC ashuhudia
******  
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Padri wa Jimbo la Kanisa Katoliki mkoa wa Mbeya amewatimua kazi na kutupa vyombo vyao nje walimu saba waliokuwa wakifundisha shule ya sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Fransisko iliyopo Forest jijini hapa baada ya kukataa kutoka katika nyumba za shule hiyo wakisubiri uamuzi wa mahakama.

Tukio hilo lilitokea Desemba 24,  mwaka huu  katika eneo la shule hiyo na kuzusha vurugu ambazo zilizimwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evance Balama aliyefika eneo la tukio na kusikiliza pande zote mbili.

Uongozi wa shule hiyo inayomilikiwa na Jimbo katoliki la Mbeya iliiomba kampuni ya Yono Auction Mart and Cout Broker tawi la Mbeya kuwatoa kwa nguvu walimu hao ambao baada ya kuachishwa kazi walifungua kesi katika mahakama ya kazi na kupewa barua na kamisheni ya upatanishi na usuluhishi ya kutoondolewa katika nyumba hizo.

Wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio walimu hao walisema kuwa chanzo cha hayo yote bu kuachishwa kazi pasipo kulipwa stahiki zao jambo ambalo lilisababisha kufungua kesi katika mahakama ya kazi.

 Walisema baada ya kufungua kesi lilitokea jaribio la kuwaondoa katika nyumba hizo ambapo Desemba 22 mwaka huu kamisheni ya upatanishi na usuluhishi kupitia mpatanishi Boniface Nyambo ilitoa zuio la kutotolewa katika nyumba hizo lakini agizo hilo likapuuzwa.

Walisema baada ya agizo hilo lenye Kumbukumbu namba CMA/MBY/158/2011 kufika kwa wamiliki wa shule hiyo, walishangaa kupata barua ya kuwaondoa kwa nguvu kupitia kampuni hiyo ya Yono.

Barua hiyo inaeleza kuwa walimu hao walioachishwa kazi walipewa taarifa ya kukabidhi nyumba hizo tangu Octoba 13, mwaka huu kupitia barua yenye kumbukumbu namba

ADV/140/2011 na kwamba kuachishwa kazi kulithibitishwa na CMA Mbeya Octoba 10 mwaka huu.

 ‘’Kutokana na walimu waliotajwa hapo chini kuachishwa kazi na kuthibitishwa na CMA Mbeya tarehe 10.10.2011. Na pia kutokana na uamuzi wa Baraza la Ardhi kuthibitisha kuwaondoa katika nyumba za shule hiyo katika uamuzi wa tarehe 22.12.2011 katika Misceleneous Application No. 7 of 2011. Tunapenda kukujulisha kwamba kampuni yako YONO AUCTION MART AND COURT BROKER imeteuliwa  kufanya kazi ya kuwaondoa kisheria mara moja walimu hao’’ imeeleza moja ya barua hiyo.

Barua hiyo imepelekwa nakala kwa walimu wote waliotajwa ambao ni  Ursula Ndeki, Simon Mapunda, Yesaya Musyani, Benezer Msangi, Leonardina Kagoro, Mary Njele na Ernest Njole.

Baada ya kampuni hiyo kuanza kutekeleza kama ilivyokuwa imepewa jukumu hilo ndipo ukaibuka mzozo kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Yono na walimu hao na familia zao hali iliyopelekea Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evance Balama kuingilia kati na kuamuru walimu hao wabaki katika nyumba hizo wakati Serikali ikijaribu kujua ukweli wa sakata hilo.

Msemaji wa shule hiyo Padri Innocent Sanga alikataa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utata huo uliokuwa umejitokeza kwa kile alichosema kuwa ni mapema kuzungumza na waandishi wa habari.

Mwanasheria wa walimu hao Ladslaus Rwekaza alisema kuwa baada ya Padri Sanga kukatalia funguo alilazimika kufungua milango mingine kwa lengo la kuhifadhi mizigo iliyokuwa imetolewa nje na kunyeshewa na mvua siku mbili mfululizo.

Na kwamba anamshangaa Padri huyo kuendesha ibada ya Krismas wakati watu anaowaongoza wakiteseka na order ya mahakama ilikuwa haijafika wakati wa kukata rufaa.

Kamanda wa polsi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alisema amesikitishwa na tukio hilo na kwamba alimwagiza Mkuu wa polisi wa wilaya kuwafungulia walimu hao lakini mpaka majira ya saa saba usiku walimu hao walikuwa bado hawajafunguliwa milango hiyo na kuwalazimu kuvunja milango.

Mbali na hilo, walimu hao wamelalamikia kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo kamera na kuharibiwa nyaraka mbalimbali za Serikali vikiwemo vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wao na vyeti vya shule.

NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI YAVAMIWA NA KUIBIWA MALI ZAKE - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:08 | 0 comments
Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya
 Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe mkoani Mbeya Bwana Thobias Mwanakatwe amevamiwa na majambazi na kuibiwa mali zake nyumbani kwake Jijini Mbeya.

 Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Mwanakatwe alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa majirani zake kuwa majambazi walikuwa wamevamia nyumbani kwake yeye akiwa safarini wilayani Kyela.

 Alisema anamshukuru Mungu yeye na familia yake hawakuwemo katika nyumba hiyo hivyo watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivunja nyumba yake na kuiba kila kitu kama hasira za kutomkuta yeye na mkewe.

Alivitaja baadhi ya vitu ambavyo watu hao waliiba ndani ya nyumba yake kuwa ni pamoja na Sub woofer mbili, Televisheni mbili,Redio aina ya Kenwood, jiko la gesi, Mtungi  wa gesi.

Vingine ni Jiko la umeme, Nguo zake zote zikiwemo suti jozi 15, nguo zote za mkewe, viatu, Magodoro, Kompyuta na vitu vingine vingi.

YALIYOJILI MKOANI MBEYA WIKI HILI

Kamanga na Matukio | 05:49 | 0 comments
 MISAADA:-Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abass Kadoro akikabidhi baadhi ya msaada kwa waathirika wa janga la mafuriko lililoathiri Kata ya Ikuti nje kidogo ya Jiji la Mbeya jana. Msaada hiyo ulikuwa ni pamoja na Blanketi 100,,Mikeka 100, Gunia 15 za mahindi na Lita 90 za mafuta. Kata hiyo ilikumbwa mafuriko ambapo zaidi ya kaya 30 zilikosa makazi ya kuishi.
 MISAADA:-Mkuu wa Wilaya Mbeya Evans Balama akikabidhi msaada wa Mchele, Mbuzi na Mafuta ya kula kwa watoto wa Gereza la watoto watukutu Jijini Meya jana kwa niaba ya rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyetoa msaada huo. (Picha na Ezekiel Kamanga).
 BAADA YA KUSHINDA KESI:- Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akizungumza nje ya mahakama ya Mkoa wa Mbeya jana muda mfupi baada ya kufutiwa kwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya kufanya mkutano kinyume cha Sheria. (Picha na Ezekiel Kamanga) 
 Mafuriko Mitaro:-Wakazi wa Kata ya Ikuti iliyopo nje kidogo ya Jiji la Mbeya wakirekebisha mtaro ambao uoliharibiwa vibaya na mafuriko yaliyoikumba Kata hiyo na kusababisha wakazi wa Kaya zaidi ya 30 kukosa makazi.
UFUNDI STADI:- Binti huyo pichani Happy Pius (9) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano ni mtoto mwenye kipaji cha pekee na kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kwa umahiri anaounesha kwa kutengeneza Pikipiki. Pichani Binti huyo akirekebisha moja ya Pikipiki iliyoletwa katika Gereji iliyopo eneo la Srereo Jijini Mbeya kama alivyokutwa na mpigapicha wetu jana.(Picha na Ezekiel Kamanga)  

MVUA KUBWA YABOMOA NYUMBA 30, MMOJA AFARIKI DUNIA , ZAIDI YA WANANCHI 100 WAKOSA MAHALI PAKUISHI JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:40 | 0 comments
Mvua kumbwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi na msaada wa haraka wa vyakula na madawa unahitajika ili kuweza kunusuru maafa. Mbali na nyumba kubomoka mvua hiyo iliyodumu kwa muda wa masaa mawili imeweza kuharibu mimea ya mazao shambani. miundombinu ua Maji, Umeme na Barabara kutokana na mafuriko.
Vitongoji vilivyoathiriwa na mvua hiyo katika kata hiyo ni pamoja na kitongoji cha Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Baadhi ya miundombinu ya maji iliyoathiriwa na mafuriko ya mvua hiyo na wananchi wakijaribu kuunganisha bomba la maji safi, Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Wanawake wakifukia shimo la choo baada ya kubomolewa na mvua kubwa iliyonyeesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti, Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Wananchi wakiendelea kutoa maji yaliyoingia katika nyumba zao zilizonusurika kubomolewa na mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
Mmiliki wa mashine ya kusaga nafaka, Bwana Mbonile Kapalata akifungua mota baada ya mashine hiyo kuingia maji kutokana na mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Juma Idd (wa pili kutoka kulia), akitoa maelekezo jana kwa kamati ya muda ya Maafa ya mtaa wa Ikuti, kuhusu kufanya tathmini ya thamani ya mali iliyoharibiwa na mafuriko ya mvua pamoja na msaada wa vyakula na madawa kwa waathirika wa maafa ya mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Baadhi ya wananchi wakitoa nje vyombo zikiwemo samani, nguo na godoro baada ya kutokea kwa mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Moja kati ya huduma muhimu katika jamii iliyoathiriwa na mafuriko, duka hili ambalo baadhi ya bidhaa zake ziliondoka na mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha  Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo.
 Mama aliyeshika tama ni mama wa marehemu Isack Sande (5) aliyefariki dunia baada ya mafuriko hayo kubomoa nyumba yao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha  Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi katika vitongoji vya Inyala, Ikuti na Maendeleo. (Picha na Mtandao huu). 

GARI YA MIZIGO MALI YA DHANDHO YATEKETEA KWA MOTO

Kamanga na Matukio | 05:42 | 0 comments
Gari ya mizigo aina ya Scania ambayo nambari yake ya usajili haikuweza kufahamika, linalomilikiwa na Kampuni ya DHANDHO ambayo hujihusisha ya usafirishaji wa mizigo mbalimbali kuanzia nchini na kupeleka nchi jirani, limeteketea kwa moto katika eneo la Chimbuya mkoani Mbeya.

KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA MWAKA TUNDUMA WAKABIDHI ZAWADI KWA WATOTO YATIMA.

Kamanga na Matukio | 05:36 | 0 comments
Mchungaji wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mwaka Tunduma mkoani Mbeya Anyandwile Kajange, akila chakula na watoto yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira hatarishi ikiwa ni ishara ya upendo kwa watoto hao, baada ya kanisa hilo kutoa nguo za sikukuu zenye thamani ya shilingi laki nane, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Bi Beatrice Mwinuka mjumbe wa Halmashauri kuu ya Jimbo ya kanisa la Moravian Tanzamia.
 Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu na hatarishi, wakisubiria kwa hamu zoezi la ugawaji wa nguo za sikukuu zenye thamani ya shilingi laki nane, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Bi Beatrice Mwinuka mjumbe wa Halmashauri kuu ya Jimbo ya kanisa la Moravian Tanzamia.
 Mgeni rasmi wa ugawaji wa zawadi kwa watoto yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira hatarishi Bi Beatrice Mwinuka(kushoto), pamoja na Mchungaji wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mwaka Tunduma mkoani Mbeya Anyandwile Kajange wakiwa wameketi kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa zawadi zikiwemo nguo za sikukuu zenye thamani ya shilingi laki nane
 Kushoto ni mtoto Julius Sikaonga mwenye umri wa miaka 2, ambaye amekuwa akilelewa na bibi huyo Bi Lucia Minga ambaye alimokota mtoto huyo Januari 18, mwaka 2009 katika mtaa wa majengo mji mdogo wa Tunduma ambapo mpaka hivi sasa mtoto huyo anaendelwea vizuri, hivyo ni mfano kwa wananchi wengine kuwa na roho yahuruma na  kusaidiana katika jamii.
 Mgeni rasmi Bi Beatrice Mwinuka akigawa zawadi kwa mmoja kati ya wajane walionufaika na msaada wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mwaka Tunduma mkoani Mbeya.
 Mchungaji Anyandwile Kajange akishuhudia zawadi zikitolewa kwa wajane, watoto yatina na waishio katika mazingira hatarishi.
Watoto hao wakila chakula kwa pamoja, licha ya kushindwa kujieleza majina yao kutokana na umri. Watoto hawa walifiwa na wazazi wote wawili hivi karibuni.

ns: WANAFUNZI ELFU KUMI WASHINDWA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA KIDATO CHA KWANZA MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 02:58 | 0 comments
Wahitimu wa elimu ya msingi katika shule ya Msingi Kambarage iliyopo jijini Mbeya wakifurahia na kushangialia baada ya kumaliza kufanya mtihani wa darasa la saba ambao umemalizika na kuwapa fursa ya kusubiria Sherehe rasmi ya Kuangwa itakayofanyika wakati wowote kuanzia sasa. Wanafunzi wengi wameshangilia na kujawa furaha kubwa.,Je? furaha hii inaweza rudiwa tena wakati wa matokeo kutangazwa.
 *****
Habari na Picha na Mtandao huu.
Wanafunzi elfu kumi mia sita na saba waliohitimu elimu ya msingi mwaka huu mkoa wa Mbeya wameshindwa kuchaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari kutokana na uchache wa vyumba vya madarasa.

Hayo yamesemwa na afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda wakati akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake na kuongeza kuwa waanafunzi hao watachaguliwa endapo ujenzi wa vyumba vya madarasa utakamilika.

Wakati huohuo amewataka wazazi kushiriki pia katika ujenzi wa ofisi ya utawala badala ya kujenga vyumba vya madarasa pekee.

Aidha Kaponda amesema kuwa wastani wa ufahulu umepanda kwa alama 13 kutoka 93 za mwaka 2009 hadi kufikia alama 106 ya mwaka 2011 ambao ni sawa na daraja la C.

BEI ZA PEMBEJEO ZA KILIMO ZAPANDA KILA KUKICHA MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 02:55 | 0 comments
Mifuko ya Mbolea aina ya DAP
*****
 Habari na Picha na Mtandao huu.
Licha ya Serikali kutunga sera yenye lengo la kumkomboa mkulima, Sera hiyo imeonekana kutokuwa na manufaa kwa wakulima kutokana na kupanda kwa bei za pembejeo za kila kila kukicha.

Wakiongea na mtandao huu baadhi ya wafanyabishara wa pembejeo za kilimo mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini wamesema kupanda kwa pembejeo hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji.

Mmoja wa wafanyabishara hao Bi.Atupele Mwakatima amesema bei ya Mbolea aina ya DAP walikuwa wakiiuza kwa shilingi elfu 37 ambapo sasa inauzwa shilingi elfu 75 Mbolea ya UREA ilikuwa ikiuzwa shilingi elfu 50 kwa sasa inauzwa shilingi elfu 65 na mbolea aina ya CAN ilikuwa ikiuzwa shilingi elfu 45 ambayo sasa inauzwa shilingi elfu 50.

Naye mmoja wa wakulima wilayani humo Bwana Fred LakimyoniI amesema kutokana na kupanda kwa gharama hizo za pembejeo kunauwezekano mkubwa wa bei ya mazao ikapanda mwakani ikiwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kushindwa kulima kilimo bora kutokana na kushindwa kumudu gharama za kununulia pembejeo za kilimo. 

WANACHUO WAGUSHI MUHURI WA BENKI, WATAFUNA ADA MILIONI 12 MKOANI MBEYA.NA

Kamanga na Matukio | 06:34 | 0 comments
Wanachuo 33 wa chuo cha Ilemi Polytechnic College wamefuja shilingi milioni 12, 450,000 za kitanzania, ada ambazo walipasa kulipa kwa ajili ya mafunzo wanayopatiwa katika chuo hicho kilichopo kata ya Iganzo jijini Mbeya.

Wanachuo hao badala ya kwenda kulipa ada hizo katika akaunti ya malipo ya shule katika Benki ya Exim, wamekuwa wakichukua stakabadhi ya malipo (pay slip) na kuzigonga muhuri ambao wameuchonga, kisha kuzipeleka stakabadhi hizo kwa mhasibu wa chuo hicho kama malipo halali ya ada.

Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto wa kike waliofanya udanganyifu huu, ambapo baada ya kubanwa na uongozi wa Benki ya Exim na chuo hicho waliweza kukiri kufanya udanganyifu huo.

Hata hivyo katika udanganyifu huo Benki hiyo haijaweza kuathiriwa na kitu chochote kwani pesa zote zipo salama, na kwamba wanafunzi hao wameathiriwa kwa asilimia kubwa kutokana na kutafuta ada zao.

Akizungumza na mtandao huu Mkuu wa chuo hicho Bwana Bon Beny Mwasaka amesema kuwa wanachuo waliofanya udanganyifu huo ni wanachuo ambao wamejiunga na masomo kwa mwaka wa kwanza, kwani chuo hicho hakijaweza kupata hasara yoyote kutokana na wengi wao kudaiwa ada na kuanza kulipa huku uchunguzi ukiendelea kufanyika ili kuweza kubaini mmiliki wa mhuri huo bandia.

Amesema kuwa wanachuo hao wameweza kugushi nyaraka za malipo ya ada kuanzia laki moja hadi laki nne na elfu themanini na kwamba atakayekamatwa kuhusika na tukio hilo la udanganyifu atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa chuo.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Exim Bwana Godfrey Kitundu amesema wamebaini kasoro zaidi ya 14 za muhuri huo, ambazo zimeonekana katika mhuri huo hivyo haikuwa rahisi benki hiyo kudanganywa na tukio hilo la kugushi nyaraka za malipo, kuwa tofauti zilizopo katika stakabadhi hizo ni pamoja na tarehe za ulipaji kuonesha ni siku ambazo benki haikufunguliwa ikiwemo Novemba 11, ambapo kulikuwepo na tukio la vurugu eneo la Mwanjelwa kutokana na benki hiyo kuwa karibu na eneo hilo pamoja na siku za jumapili.

Hata hivyo ametoa ushauri kwa chuo hicho kufuatilia mara kawa mara maendeleo ya akaunti yao ya chuo ili kubaini mapema matatizo kama hayo yaliyojitokeza na kwamba wataendelea kutoa ushauri mara kwa mara ili kuhakikisha pesa za chuo zinakuwa salama.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa chuo hicho Bwana Elton Mwamasika amewataka wanachuo kulipa mapema kiasi cha ada wanachodaiwa, endapo watachelewesha ulipaji huo basi huenda wakasimamishwa kuendelea na masomo, lakini mtandao huu uliweza kushuhudia wanachuo hao wakilipa da zao ka kuruhusiwa kuingia katika vyumba vya mitihani.

Chuo hicho hutoa mafunzo ya kilimo, biashara na kompyuta(ICT) kwa gharama ya shilingi laki 7 ambazo ni gharama za kila mwanachuo mmoja kwa hatua ya cheti na diploma.





WAFUNGA BARABARA BAADA YA MKAZI MMOJA KUGONGWA NA GARI NA KISHA KUFARIKI - MBARALI

Kamanga na Matukio | 05:58 | 0 comments
Pikipiki nambari T 156 BRE iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Abinel Maliva iligonga kwa nyuma gari nambari T 605 BBK aina ya Toyota RAV4 iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Juma Abubakari katika eneo la Esso jijini Mbeya. 
 *****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Wananchi wa kijiji cha Ilongo, wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya walifunga barabara kuu ya Mbeya - Iringa jana kwa muda wa masaa mawili, baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho kugongwa na gari aina ya roli na kisha kupoteza maisha.

Marehemu aliyefahamika kwa jina la Magreth Tito (19), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mapo Ruiwa, majira ya saa 6 mchana baada ya kugongwa na roli hilo lenye nambari za usajili T. 204 BNC lililokuwa na tela lenye nambari T 319 AYK ambalo dereva wake hakuweza kufahamika kutokana na roli hilo kutosimama baada ya kusababisha ajali hiyo.

Baada ya ajali hiyo kutokea wananchi wa kijiji hicho walitoa taarifa kituo cha polisi, lakini kutokana na Jeshi la polisi kuchelewa kufika wananchi hao walizua magari kutoendelea na safari baada ya kupanga magogo na mawe barabarani kwa lengo la kuzuia mwili wa marehemu usipondwe na magari mengine.

Kumekuwepo na ajali nyingi eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi eneo hilo kwani limekuwa likitumika kama kituo cha mabasi makubwa na madogo na hivyo kuiomba Serikali kuweka matuta, licha ya kuwepo kwa vibao vyenye ishara ya kupunguza mwendokasi lakini madereva wamekuwa wakipuuza.

Hata hivyo baada ya dereva huyo kukimbia, alilitelekeza roli hilo katika kituo cha mafuta kilichopo Igurusi wilayani humo, ambapo chanzo kimetanjwa kuwa mwendokasi wa gari hilo.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na hivyo jeshi lake kuweza kudhibiti hali hiyo ya wananchi kufunga barabara na hivyo kuruhusu magari kuendelea na safari majira ya saa nane mchana.

Ameongeza kuwa pikipiki nambari T 156 BRE iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Abinel Maliva iligonga kwa nyuma gari nambari T 605 BBK aina ya Toyota RAV4 iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Juma Abubakari katika eneo la Esso jijini Mbeya.

Dereva huyo wa pikipiki alikuwa katika hali ya mwendokasi alishindwa kuimudu pikipiki na hivyo kugonga kwa nyumba kioo na kupasuka ambapo alijeruhiwa kichwani na puani hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa jijini hapa mpaka mauti yalipomfika.


NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI ATEKELEZA AHADI YA UJENZI WA MAKTABA JIMBONI KWAKE MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:23 | 0 comments
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Mheshimiwa Philipo Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Songwe wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
*****
Na, Gordon Kalulunga, Mbeya.
Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini Philipo Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe wilayani Chunya mkoani Mbeya, ameendelea kutekeleza ahadi zake kwa kujenga maktaba ya wilaya ya Chunya jimboni humo.

Mulugo ametekeleza ahadi hiyo ikiwa ni miezi miwili kupita baada ya kuzipatia vitabu vya ziada na kiada shule za Sekondari Jimboni humo huku akiwapatia Kompyuta ndogo (LAPTOP) waratibu elimu wakata zilizopo Jimboni humo kwa ajili ya kuendeleza elimu.

Akizindua maktaba hiyo iliyopo eneo la kata ya Mkwajuni juzi, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema kutokana na watanzania wengi kutokuwa na tabia ya kujisomea, hivyo umefika wakati kubadilika na kuanza kujenga kasumba ya kujisomea machapisho mbalibali kutokana na huduma hiyo kusogezwa vijijini.

Alisema wananchi lazima watambua kuwa wanaposoma vitabu wanazungumza na watu wenye ubongo wa hali ya juu ambao walikaa na kuamua kutunga, hivyo kupitia vitabu hivyo watapata maarifa mapya ambayo yatawasaidia kuinua maisha yao katika sekta kwa mfano ya kilimo, afya, biashara nk.

Alisema  wananchi wa wilaya ya Chunya waitumie maktaba hiyo kujisomea machapisho mbalimbali ambayo ndani yake kuna maarifa ya kisasa, kijamii, kielimu, kiuchumi na teknolojia ambavyo vyote hivyo vitaweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Sanjari na hayo alisema kuzinduliwa kwa maktaba katika wilaya hio ni jambo muhimu kwani wilaya 17 pekee ndizo zenye maktaba kati ya wilaya zaidi ya 142 za Tanzania Bara ambapo wilaya ya Chunya tayari imeingia katika historia hiyo ya kuwa na maktaba inayoendeshwa kwa ushirikiano wa kati ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania na Halmashauri za wilaya.

Kandoro pia alitumia fursa hiyo kumfagilia Mbunge wa  Songwe wilayani hapa, Phillipo Mulugo kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jimbo lake kuliletea maendeleo hususani katika sekta ya elimu na kwamba wananchi wa wilaya hiyo wamuunge mkono kwa kuhakikisha wanasoma ili waweze kuinua hali zao za maisha.

Alisema Mulugo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini kazi hiyo anayoifanya mfano katika sekta ya elimu lazima aungwe mkono kwani malengo yake makuu ni kuwasaidia wananchi ili waondokane katika hali ya ujinga.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba nchini Dk.Alli Mcharazo, alisema Mbunge wa Songwe wilaya Chunya, Mulugo ndiyo chanzo cha kuomba kuanzishwa kwa maktaba ya wilaya ya Chunya ambayo baada ya kufunguliwa imeingizwa kwenye mtandao wa maktaba nchini.

Dk.Mcharazo alisema maktaba hiyo imepewa jumla ya vitabu 2034 vya masomo yote na kwamba sasa jukumu limebaki kwa wananchi kuitumia maktaba kujisomea ili waweze kupata maarifa yatakayowasaidia kupata maendeleo ya haraka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro, alimshukru Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philipo Mulugo kwa jinsi alivyopigania hadi kupatikana kwa maktaba hiyo na kamba uongozi wa wilaya utahakikisha unawahamasisha wananchi wajenge utamaduni wa kujisomea.

Akizungumza kwa njia ya simu, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Philipo Mulugo abaye hakuwepo eneo la tukio la ufunguzi wa Maktaba hiyo alisema kuwa ameamua kujikita kwanza katika elimu ambapo alisema atatekeleza ahadi zake zote.

MAFANIKIO KATIKA UENDESHAJI WA CHUO CHA UFUNDI CHA MORAVIAN(MVTC) - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:35 | 0 comments
Mgeni rasmi wa mahafali ya 11 ya chuo cha Ufundi (MVTC) kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi  Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimolo akipokea zawadi ya samani, aina ya meza iliyobuniwa na kutengeneza na wahitimu hao katika mahafali  yaliyofanyika Desemba 16 mwaka huu, katika Ukumbi wa Chuo hicho eneo la Kadege, Forest ya zamani jijini Mbeya. 
 *****
Habari na Mtandao huu.
 Wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Kanisa la Moravian Tanzania(MVTC) Jimbo la Kusini Magharibi, Mkoani Mbeya wametakiwa kutumia weledi wao walioupata chuoni hapo kwa mandeleo ya Tanzania.
 
Akihutubia katika Mahafali ya 11 ya Chuo cha Ufundi, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Gabriel Kimolo amesema wahitimu wengi hapa nchini wanapimaliza elimu zao huonekana kuwa na vyeti vya nguvu lakini ukifuatilia utendaji wao kazi ni mdogo.

Mheshimiwa Kimolo amesema, inapofikia hatua hiyo jamii hujikuta katika lindi la umaskini kutokana na kuwa na watu wengi wamesoma lakini utendaji wao ni mdogo.

Pia Kimolo amesema makampuni mengi ya nje yamefikia mahali pa kuajiri watu wa kutoka makwao na sio watanzzania kutokana na juhudi na ufanisi katika kazi hizo na kuwaacha watanzania wakilalama kwa njaa ya ajira.

Hata hivyo amelitaka Kanisa la Moravian Tanzania kama kweli lina nia ya dhati ya kuisaidia jamii ya watanzania basi inapaswa kupanua chuo hicho kwa kuomba maeneo mengine ili kusongeza huduma kwa wananchi.

Aidha amelitaka kuomba ekari zaidi ya 100 ili kuweza kuikidhi haja ya kuwasaidia watanzania wa leo na wa kizazi kijacho badala ya kuwaachia wawekezaji wa nje maeneo makubwa ya ardhi kwa uwekezaji wa makampuni yao.

Mahafali hayo ni ya 11 ambapo wahitimu 167, wavulana 61 na wasichana 106 ambapo Mkuu wa Wilaya huyo amewakabidhi tuzo wanafunzi waliofanya vizuri katika kadhia mbalimbali ikiwemo nidhamu, usafi, masomo ya uhazili.
 
 Mkuu wa Chuo cha Ufundi(MVTC) kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Bwana Gurd Lwinga akitoa utambulisho katika mahafali ya 11 ya wahitimu wa chuo hicho yaliyofanyika Desemba 16 mwaka huu, katika Ukumbi wa Chuo hicho eneo la Kadege, Forest ya zamani jijini Mbeya amesema chuo hicho hutoa mafunzo ya Ushonaji nguo, Useremala, utengenezaji wa Umeme wa sola, umeme wa majumbani, uhaziri, hoteli, kompyuta na kozi za lugha ya kiingereza. 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa  VETA kanda ya nyanda za juu kusini Bwana Justine Luta amewataka wahitimu kwenda kutangaza vema sifa ya chuo hicho kwa kuhudumia vizuri wateja na kutengeneza samani bora zenye kuvutia na serikali inaunga mkono juhudi zinazofanya na kanisa la Moravian kwa juhudi wanazozitoa kwa vijana kuwapa mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa vyuo vingine vinavyomilikiwa na Veta.

Naye Katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Mchungaji Daudi Msweve, amesema kanisa lake linawawezesha kupata vitendea kazi wanavyuo wanaohitimu ambapo jana walitoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 5,638,000 kwa wahitimu 167. 

Chuo hicho kimesajiliwa mwaka 2000 kikianza na wanafunzi 16 na namba ya usajili ni VTC/323/2002 na hakina ubaguzi wa dini, ukabila na ujinsia. Pia kuna asasi ambazo huleta watoto yatima kupewa mafunzo kama vile YWCA, NSALAGA na OAK - TREE ambazo husaidia kupunguza wimbi la watoto wa mitaani.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger