KWANZA KABISA WANAANZA TOA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA NA KUZANIWA AMEROGWA NA ALIYEZIKWA AKIWA HAI MAANA KATIKA KABURI HILO WALIZIWA WATU WAWILI KATIKA KABURI MOJA ALIE HAI NA MFU |
JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA TAYARI LIMETOLEWA HILO PEMBENI SASA ANAFUKULIWAALIEZIKWA HAI |
HII MITI NDIYO ILIYOTENGANISHA JENEZA NA ALIEZIKWA AKIWA HAI KWANZA ALIANZA ALIE HAI KUZIKWA IKAFUATIA MITI HIYO NDIYO LIKAFUATA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA |
MDOGO WA MAREHEMU ALIEZIKWA AKIWA HAI |
MWILI WA ALIEKUFA KWA UGONJWA ULIZIKWA TENA NA WANAUSALAMA KUONDOKA NA MWILI ALIEZIKWA AKIWA HAI |
WANANCHI HAO HAIKUTOSHA BAADA YA KUMZIKA MWENZAO AKIWA HAI WALIKWENDA KUCHOMA NYUMBA YAKE |
NA KUHARIBU MAZAO YAKE SHAMBANI |
Katika hali isiyokuwa ya kawaida
wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamemzika
Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja
kijijini hapo.
Tukio hilo la kusikitisha
lilitokea jana majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini
baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria
mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo, Thobias Ismail alisema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa
matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
Alisema wakati taratibu za
mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu
kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za
kishirikina.
Aliongeza kuwa wakati kaburi
likichimbwa kwa ajili ya kumzika
marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila
wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa
wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
Kutokana na mwito huo walifika
wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na
kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia
kaburini huku akisindikizwa na marungu.
Baada ya Mzee huyo kupoteza fahamu Vijana hao walianza kutandika
fito ndani ya kaburi kisha kufukia kwa udongo kiasi kwa lengo la kutenganisha
na Mwili wa Marehemu Pita uliokuwa kwenye jeneza baada ya kuwazika kwenye
kaburi moja.
Baada ya kukamilika kwa zoezi
la mazishi kundi la vijana lilielekea hadi nyumbani kwa Mzee aliyezikwa akiwa
hai na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kutotoa siri wakidai Siri ya Jeshi.
Hata hivyo baadhi ya wananchi
walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Credo
Kayanza ambaye pia alitoa taarifa kwa Diwani wa Kata hiyo Chesco Ngairo ambao
kwa pamoja walitoa taarifa Jeshi la Polisi ambao baada ya taarifa hiyo walifika
eneo la tukio huku wakidhani lililotokea ni kuchomwa kwa nyumba pekee.
Jeshi la Polisi baada ya
kufanya upelelezi na kubaini kitendo hicho waliwaamuru baadhi ya Vijana kufukua
kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya Vijana hao kulipwa.
Baada ya kufukuliwa kwa kaburi
hilo Mwili wa Marehemu Mzee Mwachirui ulichukuliwa na kupelekwa katika
Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya Uchunguzi huku Mwili wa Pita
ukizikwa upya palepale.
Baada ya kukamilika kwa
uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo
Marehemu alizikwa katika eneo tofauti na alipokuwa amefukiwa awali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Diwani Athumani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo pia ametoa wito na
kuwaasa wananchi na jamii kuacha
tabia ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi
kwa madai kuwa hauna faida kwao bali huchochea migogoro katika jamii zao.
Aidha ameongeza kuwa wakumbuke
kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria ambapo pia amewaomba wenye taarifa za walipo waliohusika
na mauaji hayo kuzifikisha polisi haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao ingawa hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment