Raisi
wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga amekabidhi santuri ya
mpango wa maendeleo ya soka, kwa lengo la kusaidia ukuzaji na kulea vipaji vya
soka kwa vijana kwa wadau wa michezo nchini ambao waliongozwa na katibu mkuu wa
baraza la michezo taifa Henry Lihaya.
Katika
hafla hiyo Tenga amesema santuri hiyo anaamini itasaidia mpango wa kukuza soka
nchini kwa kuwashirikisha viongozi wa serikali pamoja na wadau wa michezo ambao
kila siku wamekua na hamu ya kuiona Tanzania inasonga mbele katika sekta hiyo.
Hata
hivyo mpango huo umeonyesha kupokelewa vyema na baraza la michezo la taifa BMT
kupitia kwa katibu mkuu wake Henry
Lihaya, ambapo amesisitiza kuendelezwa kwa mikakati ya usaidizi wa kulea na
kukuza vipaji kwa vijana ambao ndio watetezi wa taifa la Tanzania siku za
usoni.
Lihaya
pia akawataka viongozi wa vyama vingine vya michezo kuiga mfumo wa TFF wa
kutengeneza njia kwa vijana ili kuiuwezesha Tanzania kuwa na dira nzuri ya
michezo.
0 comments:
Post a Comment