Pages


Home » » HATIMAYE WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) RUIWA MBARALI MBEYA AMBAO MBEYA YETU ILI RIPOTI KUWA WANAITAJI MSAADA SASA WAANZA KUSAIDIWA

HATIMAYE WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) RUIWA MBARALI MBEYA AMBAO MBEYA YETU ILI RIPOTI KUWA WANAITAJI MSAADA SASA WAANZA KUSAIDIWA

Kamanga na Matukio | 02:32 | 0 comments



Katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, William Simwali akimkabaidi mafuta ya kuzuia mwanga kwa mmoja ya wazazi wa watoto albino wa wilaya ya Mbarali bwana Usaje Mwambije makabidiano hayo yamefanyika katika ofisi ya Mbeya yetu jijini Mbeya

Katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, William Simwali akielezea umhimu wa kuwajali albino katika jamii
Mzazi wa watoto albino akimshukuru katibu wa chama cha albino mkoa wa Mbeya kwa msaada wao kwa watoto wao walioko huko Mbarali

Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akimsikiliza katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya mara baada ya kukadhi mafuta hayo

Mtoto Joshua akiwa darasani na wenzake 

Mtoto Linah akiwa darasani


SIKU chache baada ya Mbeya yetu  kuripoti habari kuhusu watoto wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) waishio vijijini kutelekezwa bila kupatiwa misaada, Hatimaye majibu yamepatikana baada ya wahusika kujitokeza na kuwapatia mafuta.

Watoto hao ambao walikuwa na uhitaji wa mafuta ya kupaka kwa ajili ya kutunza ngozi zao pamoja na miwani na kofia hatimaye  wamepatiwa msaada wa mafuta yenye thamani ya Shilingi Elfu Sitini(60,000/=).
  
Akikabidhi msaada wa mafuta hayo ambayo huzuia mwanga wa jua usiumize ngozi zao yaitwayo SunStop 30 ulikabidhiwa na Katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, William Simwali kwa baba  mzazi wa watoto wenye ulemavu wa ngozi.
  
Katibu huyo alisema mafuta aliyotoa yanatakiwa kutolewa bure kwa wenye mahitaji ambapo aliongeza kuwa kila yanapoisha wanatakiwa kutoa taarifa ili waweze kupatiwa mafuta hayo kwa ajili ya usalama wa ngozi zao ili isishambuliwe na mwanga wa jua.
  
Kutokanana msaada huo, Katibu huyo alitoa Vichupa vitano kwa ajili ya watoto wawili wanaosoma katika shule ya Msingi Motomoto iliyoko katika Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.
  
Simwale alisema Changamoto wanayokabiliana nayo ni namna ya kuwafikia Albino kule waliko kwa ajili ya kuwapatia vifaa na mahitaji yao kutokana na kutokuwa na usafiri ambapo wengi wao hawakai eneo moja hivyo inakuwa vigumu kuwafikia.
  
Alisema kutokana na changamoto ya usafiri inayowakabili wamekuwa wakiwatumia Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ambao hupewa dawa kulingana na idadi ya Albino katika Wilaya yake lakini wamekuwa wakishindwa kurudisha majibu kama walifika na kukabidhi dawa hizo kwa wahusika.

“ Maofisa maendeleo ya jamii wa kila wilaya ndiyo tunaowapa dawa hizo lakini tatizo hawaturudishii mrejesho wanapokuwa wamefikia na idadi ya Albino wanayokuwa wamewapatia” alisema katibu huyo.

Aliongeza kuwa alipojaribu kufuatilia kwa maofisa hao alibaini kuwa hawapeleki kabisa kutokanana yeye mwenyewe kutoletewa kutoka katika Wilaya yake ambayo anayehusika anakuwa amekabidhiwa na kuahidi kulipeleka kwa wahitaji.
  
Alisema alipojaribu kuwauliza wahusika kwa kutofika kwa wakati kupeleka mafuta hayo ambayo husaidia kuimarisha ngozi za walemavu lakini wameishia kudai kuwa hawana bajeti wala usafiri kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo.
  
Mbali na hilo katibu huyo aliongeza kuwa katika Shule zote ambazo Albino wanasoma Walimu na wasimamizi waelewe kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuvaa suruali ili mradi inaendana rangi na sare ya shule husika kwa ajili ya kuzuia mwanga wa jua ambao huharibu sana ngozi.
  
Pia alisema hata kwenye maandishi ya kawaida waowanatakiwa kukuziwa kutokana na kuzaliwa wakiwa na uwezo mdogo wa kuona ikiwa ni pamoja na kuwapa kipaumbele cha kukaa sehemu ambayo anaweza kusoma vizuri na kuwa jirani na ubao.
  
Simwali alisema katika Mkoa wa Mbeya wenye Albino 263 katika kata 114 kati ya kata 217 kwa Mkoa mzima wanahitaji msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamalia wema kwa kuwapatia misaada kama Miwani, kofia na mafuta.
  
Alisema Wilaya ya Mbozi ndiyo inayoongoza kwa kuwa na Albino wengi ambao ni 72, Rungwe 52, Kyela 16, Chunya 35, Mbeya Jiji 19,Mbarali 16, Mbeya Vijijini 48 na Ileje 8 kutokana na Takwimu iliyofanyika Mwaka 2011.


Kwa upande wake Mzazi wa watoto wenye ulemavu wa Ngozi Usaje Mwambije, aliyepokea msaada huo kwa ajili ya watoto wawili ambao ni Linah na Joshua wanaosoma Shule ya Msingi Motomoto kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa alikishukuru chama cha Albino kwa msaada wa mafuta.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger