Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
NAIBU Waziri na Mafunzo ya
Ufundi, Philipo Mulugo amewajia juu wanaotaka yeye na Waziri wa Elimu Dk.
Shukuru Kawambwa kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na matokeo mabaya ya kidato
cha nne kwa kile alichodai wanaosema hivyo hawajui mfumo wa uongozi ulivyo.
Mulugo aliyasema hayo juzi
wakati akizungumza na Umoja wa Wamiliki, Mameneja na Wakuu wa Vyuo visivyokuwa
vya Kiserikali ambapo alisema watu hao hawajui Nyadhifa za Waziri na Naibu
Waziri kuhusu wajibu wao pamoja na sekta
zingine kama Tamisemi ambao na Wamiliki wa Vyuo.
Mulugo alisema Kazi ya Waziri
na Naibu wake ni kusimamia Sera za Elimu na si vinginevyo na kuongeza kuwa
jukumu la Walimu na wanafunzi na namna ya ufundishaji iko katika ngazi zingine
ambayo ni Tamisemi na idara ya ukaguzi wa Shule.
Alisema Kazi yake yeye ni
kuajiri Walimu na kuwakabidhi kwenye Halmashauri ambazo ziko chini ya Wizara ya
Tamisemi hivyo suala la yeye kujiuzulu limeingizwa kisiasa kutokana na kulengwa
watu wawili tu na kuziacha Sekta zingine.
Aliyataja baadhi ya mambo
ambayo yamechangia kufeli kwa wanafunzi kwa kiasi kikubwa kumetokana na Wizara
ya Elimu pamoja na baraza la Mitihani kuziba mianya na udanganyifu wa baadhi ya
Walimu na Wamiliki wa Shule kununua Mitihani kabla haijafanyika.
Alisema baada ya kuziba mianya
hiyo atakayebainika kufanya hivyo watafungiwa Shule zao ikiwa ni pamoja na
kuchukuliwa Hatua za Kisheria kwa kupelekwa mahakamani na kufukuzwa kazi kwa
wahusika.
Alitaja Sababu zingine kuwa ni
Nidhamu kupungua kwa wanafunzi ambapo wanafunzi wanafika Shuleni kwa muda
wanaoutaka ikiwa ni pamoja na kumiliki simu ambazo zinasababisha wanafunzi
kujikita katika mitandao ya kijamii zaidi nakushindwa kuzingatia masomo.
Alisema ili nidhamu iweze
kurudi na wanafunzi waweze kusoma kwa bidii ni kurudisha adhabu ya viboko au
nyingine ambayo itasaidia wanafunzi kupenda Shule na kusoma kwa bidii na
kuongeza kuwa Sera ya adhabu inabidi iangaliwe upya ili kurudisha Heshima ya
Elimu kama ilivyokuwa awali.
0 comments:
Post a Comment