Warembo walioshiriki shindano
la kumtafuta Mwanamitindo bora wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wamewalalamikia
waandaaji wa Shindano hilo kwa kuwapa zawadi finyu tofauti na walivyokuwa
wameahidiwa kabla ya kuanza mashindao.
Mashindano hayo yalifanyika Machi
30, Mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya
yaliyoandaliwa na kampuni ya Tanzania Youth Arise kutoka Dar Es Salaam na
kuhusisha wasichana 25.
Malalamiko ya warembo hao
yanatokana na zawadi walizopewa washindi kuwa kiduchu tofauti na walivyoahidiwa
kabla ya kuanza mashindano ambapo inadaiwa kuwa mshindi kwanza alitakiwa kupewa
zawadi au kitu chenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki mbili
(1,200,000/=) lakini mwisho wa mashindano mshindi wa kwanza alipewa Kompyuta
ndogo (Mini Laptop) inayokadiliwa kuwa na thamani ya Shilingi Laki nne na nusu(
450,000/=).
Wakizungumza na gazeti hili
baada ya kukamilika kwa mashindano hayo Warembo hao walisema Zawadi hizo haziridhishi kutokana na
maandalizi waliyoyafanya ambapo mbali na mshindi wa kwanza kupewa kitu hicho
pia msindi wa pili alipewa Seti moja ya meza ya chakula yenye thmani ya
Shilingi Laki nne (400,000/=).
Msindi wa tatu hadi mshindi wa
tano wote kwa pamoja na washindi wa kwanza na
pili walipewa zawadi za Mkusanyiko wa mapambo ya kike kutoka kampuni ya
Oriflame ambayo thamani yake haikujulikana
huku washiriki wengine 20 walionekana kusuasua katika Hotel ya Manyanya
waliokuwa wameweka kambi kutokana na kutopewa kifuta jasho chochote.
Jullieth Sillo (20) ambaye
aliibuka mshindi wa kwanza alisema licha ya zawadi kutokuwa za uhakika lakini
ubabaishaji unaonekana uko kwa waandaaji ambao walishindwa kujipanga mapema
ambapo waliahidi kutoa zawadi ambazo hawakuwa na uhakika nazo.
Aliongeza kuwa wakati mwingine
wadhamini wanatakiwa watoe fedha na vitu mapema kabla ya kuanza kwa mashindano
na matangazo ambapo alisema wanatangazwa sana tofauti na vitu wanavyotoa
mwishoni au siku ya mashindano.
Mbali na hilo Mshindi huyo
alisema ukumbini alikabidhiwa Fedha taslimu shilingi Laki tano kiasi ambacho
alipokonywa na mratibu wa mashindano hayo kwa kilichidaiwa kuwa haikuwa sehemu
ya zawadi bali alikuwa anakamilisha sehemu ya mkataba wa udhamini ambayo
ilitolewa na kampuni ya Pepsi.
“ Kuhusu kambi ilikuwa ni nzuri
maana tumejifunza mambo mengi ambayo ni ushirikiano na watu kufanya huduma za
kijamii pamoja na kujitambua” alisema Lilian WilBroad ambaye alikuwa mshindi wa
pili.
Kwa upande wake Mratibu wa
mashindano hayo Bahati Mwakalinga, alipotafutwa ili kujibu tuhuma hizo za
kuwapokonya zawadi washindi pamoja na kutoa kiwango kisichoridhisha kwa
washiriki na washindi alisema tatizo hilo ni kweli limejitokeza lakini
halikusababishwa nay eye bali ni wadhamini walioshindwa kutoa kile walichokuwa
wamekiahidi.
Alisema sababu nyingine
inatokana na watu kushindwa kuingia kwa wingi ukumbini hali iliyosababisha
kupata kipato kidogo Mlangoni hivyo kushindwa kumudu gharama mbali mbali kama
kutoa kifuta jasho kwa washiriki wote ambao walitakiwa kupewa kila mmoja
Shilingi 25,000/= lakini kutokana na kukosa fedha Mratibu huyo aliwaahidi
washiriki kutumia fedha hizo baada ya Wiki mbili.
Alisema suala la wadhamini ni
gumu na ndiyo waliochangia kuvuruga utaratibu ambapo wamekuwa wakitoa ahadi
kubwa lakinimwisho wa siku wanashindwa kutekeleza kile wa;lichokiahidi mwanzoni
kabla ya Mashindano.
Mwakalinga aliongeza kuwa
baadhi ya zawadi siyo rafiki kwa washiriki ambao wengi wao ni wanafunzi ambapo
Msindi wa Pili ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) tawi la Mbeya
ambaye alikabidhiwa seti moja ya meza ya Chakula ambayo haitamsaidia kama
Mwanafunzi.
Aliwataja washindi kuwa ni
Mshindi wa Kwanza ni Julieth Sillo kutoka Mbeya, wa pili ni Dinah James Kutoka
Mbeya, wa tatu ni Herieth Ferera kutoka Mbeya , nne Lilian Wilbroad kutoka
Mbeya na nafasi ya tano ilichukuliwa na Karesma Fredy kutoka Katavi.
Aliwataja wadhamini kuwa ni
Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi, Access Computer Limited waliotoa zawadi kwa
mshindi wa kwanza, Global Star waliotoa zawadi kwa mshindi wa Pili ya meza ya
chakula( Coffee table) na Oriflame waliotoa bidhaa za mapambo ya wanawake kwa
ajili ya washindi wote watano.
0 comments:
Post a Comment