Wito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha
wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala ya kukubali kupandikizwa chuki na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Scourt Mkoa wa mbeya Ndugu Pablo Sanga akizungumza na
waandishi wa habari jijini humo amesema kuwa kuna kila sababu ya wananchi
mkoani humo kuilinda amani ya mkoa huo ilikuvutia shughuli za kimaaendeleo .
Amesema katika kipindi cha hivi
karibuni kumekuwepo na matukio
mbalimbali yanayoashiria kuvuruga amani ya mkoa huo hivyo nivema wananchi wa
mkoa huo wakawa makini na baadhi ya watu wanaopandikiza chuki zidi ya viongozi wao na serikali yao
kwa ujumla.
Pablo amesema siasa chafu zinazo enezwa
na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini ndizo zitakazo weza kusababisha madhara
ambayo ndiyo yatakayo changia kuvuruga kwa amani ambayo imedumu kwa muda mrefu
sasa.
Kauli hiyo ya kiongozi wa scourt mkoani
humo imekuja kufuatia kuwepo kwa ujio wa kiongozi wa kitaifa Rais Kikwete
ambaye anatarajiwa kufanya ziara ikiwa ni pamoja na kuzungumza katika sherehe
ya mei mosi kitaifa ambayo itafanyika mkoani hapa.
Hata hivyo Kiongozi huyo wa Scourt
amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanampokea vyema Raisi Kikwete katika
kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anafanya ziara yake kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa vitendo viovu.
0 comments:
Post a Comment