Pages


Home » » MAUAJI YA KUTISHA RUNGWE

MAUAJI YA KUTISHA RUNGWE

Kamanga na Matukio | 02:32 | 0 comments

KUSHOTO  NI BABA MZAZI WA AYUBU AGEN MWAKALEGELA AKIWA NA NDUGU ZAKE WAKISUBIRI KUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU AYUBU
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZINAZOONEKANA ZA MTOTO AYUBU HAPA NICHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU
MWILI WA ALIYETUHUMIWA KWA MAUAJI YA MTOTO AYUBU AGEN UKIWA UMECHOMWA MOTO NAWANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMKUTA MITA CHACHE KUTOKA KWENYE MWILI WA MAREHEMU AKIWA NA KISU KINACHODHANIWA KUTUMIKA KATIKA MAUAJI
MWILI WA MTOTO AYUBU UKITOLEWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANAWILAYA YA RUNGWE
SAFARI YA KUELEKEA KIJIJI CHA IJOKA KWA MAZISHI

-wananchi wapanda hasira wamteketeza kwa moto mtuhumiwa.

MATUKIO ya kutisha na ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya kummbana ili aeleze sehemu  walikokificha kichwa cha marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.
Habari za uhakika kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ijoka  katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda,  zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti  huyo alisema,  marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba nyumbani kwao.
Mwaikenda alisema  mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu .
“Marehemu alichukuliwa na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na wenzake baada ya kuona hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi walianza kumtafuta bila mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea na harakati hizo waliukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa kichakana na wauaji hao kuondoka na kichwa” alifafanua Mwaikenda.
Mkazi mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia mashaka.
Alisema baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo hapo.
Hata hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo licha ya kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu huyo hakijaonekana  na jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki mauaji hayo naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira  ambao licha ya kumuua waliuteketeza mwili wake kwa moto”.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 35  na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa  na imani za kishirikina.
Wakati huo huo watu watatu  wamefariki dunia  na wengine wawili kujeruhiwa vibaya,  katika matukio mawili tofauti ya ajili za barabarani mkoani hapa.
Katika tukio la kwanza lililotokea eneo la Mbalizi wilayani hapa, majira ya saa nne usiku  katika barabara ya Mbeya- Tunduma, watu wawili, Meshaki Inkuru (24) na Said Ndasi (19) baada ya gari aina ya Toyota Chesser yenye nambari  za usajili T 516 AAA lililokuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika  kuwavamia wakiwa nje ya Hoteli ya Royal Tughimbe walikokuwa wakiendelea na sherehe za Pasaka.
Kamanda wa polisi aliwataja majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali teuli ya wilaya ya Mbeya ya Ifisi ni Shar Mkumbwa (20), Juliet Katemi (18)   wote wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi.
Tukio lingine  ni lile lililotokea eneo la Soweto ambapo mtu mmoja mtembea kwa miguu, aliyetambuliwa kwa jina moja la Paul (60) kufa papo hapo baada ya kugongwa na gari ambayo hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja .
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger