Na Shaban Kondo.
Hatimae kiungo kutoka nchini Ivory Coast Yaya
Toure amemaliza mvutano na uongozi wa klabu ya Man City, baada ya kukubali
kusaini mkataba wa mika minne ambao
utamuwezesha kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya mjini Manchester nchini
Uingereza.
Taarifa zilizochapishwa katika mtandao wa klabu ya
Man City zimeeleza kwamba mvutano uliokuwepo baina ya kiungo huyo mwenye umri
wa miaka 29, haupo tena na sasa Yaya Toure ataendelea kuwepo Etihad kwa furaha
na amani.
Taarifa hizo zimeeleza kubainisha kwamba mkataba wa
miaka minne uliotiwa saini na mchezaji huyo ambae amekua muhimili mkubwa wa
kikosi cha Roberto Mancini, utamuwezesha kulipwa kiasi cha paund million 11 kwa
mwaka hatua mbayo imempandisha na kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoendelea
kulipwa mshahara mkubwa klabuni hapo.
Hata hivyo taarifa za Yaya Toure
kuwa mbinu za kusaini mkataba mpya tayari zilikua zimeanza kuandikwa kwenye
vyombo vya habari ambavyo vilimnukuu wakala wake Dimitri Seluk ambapo alidaiwa kuwaonya viongozi wa klabu ya Man
City kuwa makini na suala la mchezaji wake na kama itakua kinyume na hapo huenda
mwishoni mwa msimu huu angeanza kampeni ya kusaka klabu nyingine.
Kutokana na maelezo hayo ya wakala
wa Yaya Toure, vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hizo viliripoti kwamba
uongozi wa Man City ulishtushwa na kauli hiyo na ndipo ulipoanza kufanya mipango
ya haraka haraka ya kuhakikisha dili la kusianiwa kwa mkataba mpya linatimizwa
kabla ya msimu huu haijafikia kikomo.
Wakati huo huo kiungo kutoka nchini Ufaransa, Samir Nasri amefungiwa kuendesha gari
akiwa nchini Uingereza kwa muda wa miezi sita, baada ya kushindwa kulipa faini
kutokana na kosa la kukutwa akiendesha gari kwa mwendokasi.
Samir Nasri ambae ni kiungo wa klabu ya Man City, ameangushiwa adhabu hiyo
ikiwa ni baada ya siku moja ambapo mashabiki wa soka ulimwenguni kote
kushuhudia ama kusikia adhabu iliyomuangukia Carlos Tevez ya kupewa siku 250 za
kuhudumia jamii na pia kufungiwa miezi sita kwa kutokuwa na bima.
Nasri mwenye umri wa
miaka 25 alipigwa faini ya paundi 1,900 lakini alifanikiwa kuiepuka baada ya
kuandika barua kuwa hakujua kwamba gari lake aina ya Mercedes lilikuwa
limekamatwa na kamera za barabarani kwa kosa la kwenda mwendokasi katika
matukio matatu tofauti.
Hata hivyo Samir Nasri
bado ana wigo wa kukata rufaa ya kupinga adhabu aliyopewa endapo ataona
hakutendewa haki.
0 comments:
Post a Comment