Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi wa dini kutoa ushauri kwa waumini
pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya mauji ya
kikatili vivavyo endelea kujitokeza siku hadi siku katika maeneo yote Mkoani
hapa yanayo hatarisha uvunjifu wa amani na kuliletea sifa mbaya jiji la Mbeya,
Kandoro
aliyasema hayo jana wakati wa sherehe za
maadhimisho ya sikukuu ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar ambayo kimkoa yalifanyika Wilayani Rungwe na kuhudhuria na viongozi
mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya,baada ya kutokea matukio
mfululizo ya mauaji ya kinyama yanayohusishwa na imani za kishirikina,
Baada ya
kutoa ushauri huo kwa viongozi wa dini,Mh,Kandoro pia alizungumzia mfumo wa
serikali mbili Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo yenye
dola inayo shughulikia Utawala,Ulinzi na
usalama na masuala yote ya muungano na mambo ya Tanzania Bara yasiyo ya
muungano,
Alisema kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina
mamlaka juu ya mambo yasiyo ya muungano yanayohusu Zanzibar tu kama ilivyoainishwa katika sehemu ya kwanza
ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho
yake,
Aliongeza
kuwa Kila mmoja wetu anao wajibu wa kudumisha umoja,mshikamano na muungano wetu
kwa kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwl ,Julius
Nyerere pamoja na Hayati Sheikh
Abed Karume ambao walipiga vita
udini,ukabila, Rushwa na aina zote za ukiukwaji wa haki za binadamu,
‘’Ndugu
zangu wana Rungwe na wana Mbeya wote tunatakiwa tuuenzi Muungano wetu pamoja na
kudumisha Amani,Utulivu,Upendo na mshikamano
miungoni mwa watanzania na majirani zetu,kupiga vita umasikini,ujinga na
maradhi, kuimarisha misingi ya Utawara bora na Demokrasia’’,alisema Kandoro,
Aidha
Kanoro
aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kupambana kikamilifu na maambukizi
mapya ya UKIMWI,kupinga vitendo vya Rushwa,na imani za Kishirikina
zinazopelekea mauaji ya
wananchi wasio na hatia,na kuwataka kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF)
ili waweze kunufaika na huduma bora za Afya kwa kuchangia fedha mara
moja tu
kwa mwaka,
Pia ailiwataka wananchi kushiriki kikamilifu
katika shughuri mbalimbali za maendeleo
ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za waalimu pamoja na ununuzi wa
madawati ili kupunguza changamoto katika shule zetu na vijana wetu waliopo
katika shule za msingi na sekondari waweze kusoma vizuri na kupata matokeo mazuri pindi wamalizapo
masomo yao.
0 comments:
Post a Comment