Nahodha wa timu ya taifa Tanzania Taifa stars Juma Kaseja
ama Juma Juma amewataka Watanzania
kuendelea kuonyesha ushirikiano na timu ya taifa kwa ajili ya kuiwezesha
kufanya vyema kwenye michuano ya kufuzu
kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Mbali na mashabiki wa soka nchini, pia Kaseja amewataka
viongozi wa serikali kushikamana na wadau wengine kwa hali na mali kwa ajili ya
kuhakikisha dhana ya mafanikio inatimia kwa timu hiyo.
Katika hatu nyingine
Afisa wa Wizara ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Charles Yesse Matoke ameungana na kipa huyo wa klabu ya Simba katika harakati
za kuhimiza umoja ambao ndio siri ya mafanikio.
Matoke amesema kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha kwa
watanzania wote dhidi ya timu yao ya taifa, kutakua na hitaji kubwa la
wachezaji kusaka ushindi wanapokua katika uwanja wa nyumbani na ugenini.
Kama itakumbukwa vyema, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dkt Fenella Mukangara alitangaza kamati ya Ushindi ya Taifa Stars ambayo
itafanya kazi na wadau wwa michezo kwa ajili ya kuhakikisha timu ya taifa
inafanya vyema kwenye michezo ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia za
mwaka 2014 ukanda wa barani Afrika.
Kuundwa kwa kamati hiyo kumeonyesha wito wa nahodha Juma Kaseja
kuitikiwa vyema na serikali ya awamu ya nne ambayo inaongozwa na Raisi Jakaya Kikwete
ambae ni mdau wa kwanza nchini kwa sasa anaependa michezo.
Kamati iliyoundwa na waziri wa habari utamaduni
na michezo hapo jana inaongozwa na Mohamed
Dewji kwa kushirikiana na Teddy Mapunda (Montage), Dkt. Ramadhani
Dau (Mkurugenzi Mtendaji NSSF), Dioniz Malinzi (Mwenyekiti BMT), Abji
Shabir (New Africa Hotel) pamoja na George Kavishe (TBL).
Wengine
ni Mohamed Raza (Zanzibar), Leodger Chilla Tenga ( Raisi TFF), Joseph
Kusaga (Clouds Media Group), John Komba (Mbunge) pamoja na Zitto Kabwe
(Mbunge).
0 comments:
Post a Comment