Pages


Home » » Naibu Waziri Philipo Mulugo anatarajia kuwafikisha mahakamani waliomchafua kuwa ameghushi vyeti

Naibu Waziri Philipo Mulugo anatarajia kuwafikisha mahakamani waliomchafua kuwa ameghushi vyeti

Kamanga na Matukio | 01:53 | 0 comments
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh, Philipo Mulugo.

Na mwandishi wetu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai ameghushi vyeti vya elimu ya Sekondari.

Naibu Waziri huyo amesema amechoshwa na kashfa hizo zilizosambazwa na baadhi ya watu wenye nia ya kumchafua jina.

Mulugo amesema kuhusu suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana amesema matokeo hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wamafunzi.

Aidha amewataka wazazi kujenga tabia ya kuhudhuria vikao vya maendeleo ya elimu katika kata zao ili waweze kujua na kujadili changamoto mbalimbali za elimu kwa watoto wao badala ya kuishia kuilalamikia Serikali.

Mulugo ametoa wito huo wakati wqa mahojiano na Chimbuko Letu, ambapo amesema kupitia mikutano ya wazazi na kamati za shule, changamoto mbalimbali zinaweza kutatuliwa kwa wakati.

\Ameongeza itakuwa ni vigumu kwa wazazi kulalamikia ubovu wa miundombinu ya shule, maendeleo mabaya ya elimu kwa watoto wao endapo hawatashiriki kikamilifu katika kufuatilia mwenendo wa masuala ya elimu yanayowazunguka watoto wao.

Wakati huohuo amehimiza wazazi kujenga ushirikiano na waalimu ili kudhibiti vitendo viovu vya utovu wa nidhamu kwa wanafunzi huku wazazi wakiishia kutoa lawama kwa Serikali.

Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger