Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wakazi wa kijiji cha Saza wilaya ya Chunya
mkoani Mbeya wamesitisha uuzwaji wa kifusi cha mchanga kwa kampuni ya uchimbaji
madini ya Shanta Mining Company Ltd kutokana na kutaka kuongezwa kwa kiwango cha fedha kilichotolewa
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kijiji cha Saza wamesema kuwa kampuni hiyo imetoa dola za
kimarekani laki mbili na hamsini elfu kununua kifusi hicho na kuahidi kulipa
dola mbili kwa kila tani hali ambayo hawakukubaliana nayo
Wamesema kiwango cha dola mbili ni kidogo
na kutaka kuongezwa dola nne kufikia sita hali ambayo mwekezaji alikataa na
kuamua kukirudisha kifusi hicho kwa serikali ya kijiji
Akiongelea suala hilo mwanasheria wa
serikali katika halmashauri ya wilaya ya Chunya Simanyani Twavusitile amesema
wanaweza kuunda kamati ya mpito kwa ajili ya kukamilisha mchakato na tathimini
ya kupata mteja mwingine kwa bei itakayokubalika.
Miongoni mwa Waliochaguliwa ni Tabia
Andembwisye,Charles Andemwisye,Shadrack Machalawe,Atuganile Njala Robert Nselu,
mtendaji wa kijiji John Ntakoma na mwenyekiti wa kijiji cha saza Philipo
Mwakitalim.
Wakati huohuo Viongozi wa serikali ya kijiji cha Saza wilaya ya Chunya mkoani Mbeya
wanatuhumiwa kuuza eneo la kijiji kwa mwekezaji wa kampuni ya uchimbaji
madini ya shanta maining bila
kuwashirikisha wakazi na halmashauri ya wilaya ya chunya
Wakizungumza na Chimbuko Letu baadhi ya wakazi
wa kijiji hicho wamesema viongozi hao waliuza eneo hilo juni 17 mwaka 2009 kwa
kiasi cha shilingi milioni mbili ambapo mwekezaji huyo amefanya eneo hilo kuwa makazi ya
kudumu
Wamesema eneo lililouzwa lina ukubwa wa
mita za mraba mia nne ambapo zimewekwa alama (BEACON)
Katika mkataba uliyosainiwa na viongozi
hao na mwekezaji huyo unaonyesha kuwa haujapitishwa kwa mwanasheria ,mkurugenzi
na raisi ambaye ndiye mwenye dhamana ya mwisho kwa uuzwaji au umiliki wa ardhi.
Viongozi wanaotuhumiwa kuuza eneo hilo ni
pamoja na mwenyekiti wa kijiji Gasper Roki Msuwila, mtendaji wa kijiji Mariaam
Mwanijembe, mjumbe wa kamati John Mpozayo
na mashahidi wawili ambao Meck Kitalawe na Christian Mambwe.
0 comments:
Post a Comment