Ujumbe wa shirikisho la soka duniani FIFA umamaliza
shughuli ya kuisikiliza malalamiko ya baadhi ya waliokua wagombea wa nafasi za
uongozi wa shirikisho la soka nchini ambao waliondolewa na kamati ya uchaguzi
pamojana kamati ya uchaguzi ya rufaa.
Ujumbe huo ambao ulikuwa chini ya mkuu wa idara ya
wanachama wa FIFA Primo Cavaro hii
leo jioni umekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia kwa kina suala hilo
ambalo litawasilishwa kwenye makao makuu ya FIFA na kisha majibu yatarudishwa
baada ya siku saba zijazo.
Primo Cavaro amesema suala walilokuja kulifanya hapa nchini
ni kubwa hivyo yeye pamoja na timu yake hawawezi kutoa majibu ya moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment