Picha na Ezekiel Kamanga & Mbeya Yetu Blog
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
ulioanzishwa Mwaka 1999 kutokana na Sheria ya Bunge kifungu namba 2 ya Mwaka
1999 inajivunia kuwa mfuko unaoongoza kwa kulipa mafao bora kwa watumishi.
Wakizungumza na Mwandishi wetu wakati wa kilele
cha Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya ambao
hawakutaka majina yao yaandikwe kutokana na maadili ya kazi yao walisema
miongoni mwa mashirika yanayotoa mafao Nchini PSPF ndilo shirika bora kuliko
yote.
Walisema ubora wa Shirika lao unatokana na
mtindo wa kulipa mafao kwa wanachama wake wastaa kwa kutumia mshahara wa mwisho
wa mfanyakazi tofauti na mashirika mengine yanayoangalia mishahara ya miezi
sita.
Walisema shirika lao linajivunia mafanikio mengi
ikiwemo ya uwekezaji uliosalama ambapo fedha za mwanachama hufanyiwa miradi
ikiwemo kumkopesha mwanachama anayekaribia kustaafu kutokana na wafanyakazi
wengi kukosa mahali pa kuishi baada ya kustaafu.
Waliongeza kuwa fedha zinazotolewa na shirika lao
zinathamani kubwa ambapo hadi kufikia Mwezi Machi Mwaka huu Shirika lina
thamani ya Shilingi Trilion 1.2 kutoka kwa wanachama zaidi ya 340,000.
Walifafanua zaidi kuwa Shirika hilo limeanzisha
mpango wa uchangiaji wa hiari kwa watumishi wasio na ajira maalumu ambapo mafao
yao yatakuwa kwenye Elimu, Ujasiliamali, Ugonjwa mirathi, mirathi na kujitoa
kazini.
Pia walisema shirika hilo limeanzisha mradi wa
ujenzi wa nyumba kwa wanachama ambao ni wamuda wa miaka mitano na kuendelea
ambapo tayari mikoa mitano imeanza kunufaika ambayo ni Dar Es Salaam, Mtwara,
Tabora, Morogoro na Shinyanga huku ujenzi ukitarajiwa kuanza katika mikoa ya
Dodoma, Mbeya, Iringa na Kilimanjaro ambako viwanja vimepatikana tayari.
|
0 comments:
Post a Comment