Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wananchi
wa Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wameulalamikia Uongozi wa Halmashauri hiyo kwa
kutowajengea Soko kwa ajili ya kufanyia biashara zao kutokana na kubomolewa kwa
soko lililokuwepo awali ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa.
Wananchi
hao waliwaambia Waandishi wa Habari kuwa Soko la Awali lilibomolewa Miaka minne
iliyopita lakini tangu kipindi hicho Serikali ya Halmashauri ya Wilaya
haijafanya juhudi zozote wala kuwaonesha sehemu nyingine ya kufanyia biashara
licha ya kusimika nguzo zinazoashiria ujenzi kuendelea kwa muda mrefu.
Walisema
hali ya biashara ni ngumu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kuuzui bidhaa
zao majumbani na wengine kuchanganya bidhaa za vyakula na vifaa vya ujenzi na
vipodozi katika duka moja hali inayohatarisha afya za wakazi hao.
Mwenyekiti
wa Soko la zamani, Emmanuel Mwaijumba alisema kutokana na kukosekana kwa soko
hakumumizi Mwananchi peke yake lakini pia Halmashauri inakosa Fedha kutokana na
kutokuwepo kwa ushuru wa soko kutoka kwa wafanyabiashara.
Alisema
kufuatia kukosekana kwa soko hilo walipeleka malalamiko yao kwa Mkurugenzi na
Mkuu wa Wilaya hiyo lakini hakuna majibu yoyote licha ya wenye vibanda
vinavyozunguka lililokuwa soko la zamani kuendelea kutozwa fedha.
Aliongeza
kuwa mbali na kubomolewa kwa soko hilo vibanda vilivyopo havina eneo la vyoo
hali inayosababisha usumbufu kwa wenye nyumba jirani na maeneo hayo kutokana na
watu wengi kuomba huduma ya choo, pia uwepo wa ghuba la taka eneo hilo
kutozolewa kwa muda mrefu ambapo zimekuwa zikichomewa hapo hapo na kuleta adha
kwa wamiliki wa Hoteli za jirani kutokana na uchafu, harufu mbaya na moshi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Deodatus Kinawiro alipo pigiwa Simu kuzungumzia
suala hilo alikiri kuwepo kwa tatizo na kuongeza kuwa suala hilo lipo kwenye
mchakato wa kushughulikiwa hivyo wananchi wawe na subira.
0 comments:
Post a Comment