Pambano
la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon
(Indomitable Lions) lililochezwa Februari 6 mwaka huu na wenyeji
Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 limeingiza sh. 148,144,000.
Fedha
hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 23,092 waliokata tiketi
kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh.
10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 22,598,237.29, maandalizi ya mchezo sh.
58,000,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,340,900.
Nyingine
ni bonasi kwa wachezaji wa Taifa Stars sh. 18,831,864.41, asilimia 20
ya gharama za mchezo sh. 8,274,659.66, asilimia 15 ya uwanja sh.
6,205,994.75 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 2,068,664.92.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,823,978.98 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,241,199
ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Shirikisho
la soka nchini TFF limetoa shukurani kwa wadau wote wa michezo waliotoa mchango
uliopelekea uliopelekea ushindi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi
ya timu ya taifa ya Cameroon hapo
Afisa
habari wa TFF Boniface Wambura
amesema hawana budi kutoa shukurani kwa wadau wa michezo nchini kutokana na
ushindi uliopatikana wa bao moja kwa sifuri katika mchezo wa kimataifa wa
kirafiiki ambao inaaminika itaisaidia Tanzania kupanda katika viwango vya ubora
wa soka duniani.
Wakati
TFF wakitoa shukurani hizo, uongozi wa klabu ya Simba nao umeipongeza timu ya
taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa kufanya vyema katika mchezo dhidi ya
Cameroon.
Afisa
habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga
amesema bila kujali itikadi za ushabiki, uongozi wa klabu hiyo umeona ipo haja
ya kuwapongeza wachezaji wote pamoja na viongozi wa benchi la Ufundi wa Taifa
Stars kufuatia jitihada walizozionyesha na kupelekea furaha kwa watanzania.
Mchezo
ulikua na lengo la kuiandaa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo
inakabiliwa na mtihani wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za
mwaka 2014, ambapo mwezi ujao itacheza dhidi ya timu ya taifa ya Morocco ili
hali timu ya taifa ya Cameroon itakabiliana na timu ya taifa ya Togo.
0 comments:
Post a Comment