Beki
wa Timu ya taifa ya Uingereza Ashley Cole akipambana na mchezaji wa
Timu ya Taifa ya Brazil Oscar. Uingereza waliibuka na usindi wa Goli 2
kwa goli moja
Habari Kamili.
Baada ya kuanza vibaya akiwa na
kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kilishindwa kuunguruma katika uwanja
wa Wimbely huko nchini Uingereza kufuatia kisago cha mabao mawili kwa moja
kilichotolewa na wenyeji, kocha mkuu wa mabingwa mara tano duniani timu ya
taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari
amesema hajaudhika sana na hatua hiyo ya kufungwa.
Luiz Felipe Scolari
ambae alikiwezesha kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kutwaa ubingwa wa dunia
mwaka 2002 huku akikiondoa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo
wa hatua ya robo fainali mwaka huo, amesema kwa sasa timu ya taifa ya Uingereza
imebadilika na hana budi kukubaliana na suala hilo.
Amesema uzuri wa kikosi cha timu ya
taifa ya Uingereza umempa changamoto kubwa ya kukifanyia marekebisho kikosi
chake, ambacho kitakua mwenyeji wa fainali zijazo za kombe la dunia kwa ajili
ya kuhakikisha kinatoa upinzani kwa yoyote watakaekutana nae kwenye fainali
hizo.
Wakati Luiz Felipe Scolari akikubalia matokeo ya kufungwa mabao mawili kwa
moja kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amekipongeza kikosi chake kwa kusema kilicheza vizuri
wakati wote huku kikifuata maelekezo yake.
Roy Hodgson
ambae anajukumu zito la kubadili mwenendo wa timu ya taifa ya Uingereza,
amesema walipambana na timu yenye vigezo vyote hivyo walichukua tahadhari
mapema kwa kujiandaa kikamilifu na mwishowe walifanikisha azma waliyokua
wameikusudia.
Wakati huo huo mshambuliaji wa klabu
ay Man Utd Wayne Rooney amesema kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza
kinastahili kujipongeza kwa ushirikiano mzuri ulioonekana kwa mashabiki wao na
pia amesisitiza hali hiyo kuendelezwa kila wanapokutana na timu yoyote duniani.
Amesema hawana budi kufanya hivyo
kutokana na soka kuwa katika mtazamo tofauti na ilivyokua siku za nyuma hivyo,
ni jukumu lao kuhakikisha wanaendeleza mshikamano walionao kwa sasa.
Mabao ya timu ya taifa ya Uingereza
katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki yalipachikwa wavuni na Wayne
Rooney pamoja na Frank Lampard katika dakika za 26 na 60 huku bao la kufutia
machozi la timu ya taifa ya Brazil likifungwa na mshambulaiji wa klabu ya
Fluminense Frederico
Chaves Guedes.
0 comments:
Post a Comment