Pages


Home » » Kesi inayomkabili Mchungaji Daniel Mwasumbi imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya.

Kesi inayomkabili Mchungaji Daniel Mwasumbi imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya.

Kamanga na Matukio | 18:49 | 0 comments
Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi anaetuhumiwa kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi akitoka mahakamanibaada ya kudhaminiwa

 Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Kesi inayomkabili Mchungaji Daniel Mwasumbi imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya ambapo utatuzi wa  kisheria  ulifanyika na hakimu wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo anyesikiliza kesi hiyo alitoa ufafanuzi wa kisheria

Ndeuruo amesema mahakamani hapo kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea mahakama kukataa  kupokea sampuli ya vinasaba DNA  ni pamoja na mtuhumiwa kutosaini katika barua ya mrakibu wa polisi , mshtakiwa kutosomewa  haki zake  kabla ya kuchukuliwa vipimo ,mshtakiwa kutokupewa nakala ya majibu kwa mujibu kifungu cha vinasaba kifungu cha 25 kifungu kidogo na cha pili  (c) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Pamoja na  Mlalaikaji Neema Ben  kutoa vielezo mahakamani ambavyo ni watoto wake Irene na  Johnson mahakama imesema haiko tayari kupokea vina saba kutokana na kutokukamilika  kwa taratibu za kisheria

Wakili wa serikali Achirey Mulisa  na wakili wa utetezi Mkumbe wamekubaliana  na hatua iliyofikiwa na hakimu wa mahakama hiyo ambapo kesi hiyo itatajwa tena march 7 mwaka huu.

Siku ya jana, sakata hilo la mchungaji DANIEL MWASUMBI limeingia katika sura mpaya baada ya mchungaji huyo kutokufika mahakani kwa kusingizia ugonjwa
akisoma hati ya  ya mashtaka mwendesha mastaka  wa mahakama hiyo ACHIREI MULISA mbele ya hakimu GILBERT NDEURUO amesema hakubaliani na hoja ya wakili wa mtuhumiwa wakili MKUMBE  kuwa mtuhumiwa ni mgonjwa licha ya kuwasilishwa cheti cha zahanati ya ebeneza  iliyoko kabwe jijini mbeya
Kufuatia taarifa hiyo wakili huyo aliiomba mahakama kuahirisha kesi  hiyo kwa muda na kuamua kufuatilia hadi katika zahanati hiyo ambapo dactari  YUSUFU YASINI SENTI alikiri kutoa cheti bila kuonana na mgonjwa ambapo hata jina halikuorodheshwa katika vitabu vya zahanati
Baada ya dactari  kukiri wakili alimuomba wakili wake pamoja na mdhamini  kumleta mtuhumiwa mahakamani mara moja ambapo aliletwa na  kesi kuendelea katika mahakama ya siri na ushaidi kuanza kutolewa
Miongoni mwa waliotoa ushaidi ni pamoja daktari aliyepima vinasaba  FIDELIS SEGUMBA  na mwanafunzi wa shule ya sekondari ITENDE ambaye anadaiwa kuzaa na mchungaji huyo  na kuleta vielelezo wakiwemo watoto wawili wa kike na wa kiume ambao  inadaiwa kuzaa na mchungaji MWASUMBI
 Hata hivyo kulizuka ubishani wa kisheria ambapo wakili  wa mtuhumiwa alipinga kupokelewa kwa vipimo hivyo mbele ya mahakama na kudai kuwa taratibu za kisheria hazikufuatwa hali iliyosababisha kuairishwa kwa kesi hiyo  ambapo kesi hiyo itasomwa tena leo na hakimu  kuwagiza upande wa serikali kuleta barua ya uthibitisho
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger