Mkuu wa wilaya ya
Rungwe Crispin Meela
Na Gabriel Mbwille, Mbeya.
Serikali wilayani Rungwe mkoani Mbeya
imesema inatarajia kuanza kutoa vocha za Ruzuku kwa wakulima kupitia vikundi
ili kukabiliana na tatizo la wizi kutoka kwa mawakala na baadhi ya watendaji wa
Serikali.
Akiongea na Mwandishi wetu Mkuu wa wilaya ya
Rungwe Crispin Meela amesema mfumo wa awali ulikuwa ukitoa mwanya kwa mawakala
kuwarubuni wakulima kwa kuwapa fedha badala ya pembejeo husika.
Kuhusu sababu ya Vocha kuchelewa
kutolewa kwa wakati Meela amesema imetokana na mahitaji ya vocha hizo
kuongezeka.
Wakati huohuo amesema Serikali
imedhamiria kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara ambao wamekuwa
wakiwalaghai wakulima kwa kununua mazao yakiwa mashambani.
Aidha amesema ili kukabiliana na tatizo
la wakulima kushawishika kuuza mazao yao yakiwa shambani Serikali imeanza kutoa
mikopo yenye masharti nafuu.
0 comments:
Post a Comment