Na, Ezekiel Kamanga Mbeya.
Wafungwa wanaotumikia vifungo
mbalimbali Mkoani Mbeya wanatembea nusu uchi kutokana na sare zao kuchakaa na
kuondoa hali ya utu wa kibinadamu hali inayoonesha Wizara ya Mambo ya ndani
haiwajali, licha ya Serikali kuonekana kuboresha maslahi kwa watumishi wake na
kuhakikisha wanavaa sare nzuri.
Uchunguzi umebaini kuwa wafungwa
katika magereza ya Ruanda, Songwe na Kawetere ndio yaliyo katika hali
mbaya na kuwafanya baadhi ya ndugu kushindwa kuwatembelea ndugu zao baada ya
wafungwa hao kushindwa kujisetiri kwa adha hiyo.
Aidha mbaya zaidi ni pale
wanapoamriwa kuchuchumaa chini hivyo wafungwa hao kuwa na mawazo ya namna ipi
waweze kujisetiri maungo yao hasa kwa wafungwa wa jinsi ya kiume.
Katika hali ya hewa mkoani hapa
ni baridi kali na wafungwa wengi hawana masweta na hivyo kubaki na sare chakavu
ambazo zinahatarisha afya zao na kuwa hatarini magonjwa ya kifua na vichomi
ambavyo vinaweza kusababisha vifo.
Wakuu wa magereza katika
magereza hayo hawakuweza kuzungumzia lolote wakidai kuwa wao sio wasemaje wa
Jeshi la magereza.
Hata hivyo juhudi za kumpata
msemaji wa Jeshi la magereza makao makuu ziligonga ukuta baada ya kuambiwa kuwa
msemaji yupo safarini na haijulikani siku ya kurudi kazini.
0 comments:
Post a Comment