Na Shaban Kondo,
Kamati ya uchaguzi ya shirikisho al soka nchini TFF
imeendelea kutupiwa lawama baada ya kukamilisha zoezi ya kusikiliza mapingamizi
yaliyowasilishwa na wadau wa michezo dhidi ya wagombea nafasi mbalimbali za
uongozi wa shirikisho hilo.
Kamati hiyo baada ya kulaumiwa na Frank Mchaki aliekua amemuwekea pingamizi Hamad Yahya Juma anaewania nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu
pamoja na Saidi Mohamed anaewania
nafasi ya makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, imeendelea kulaumiwa na Paul Muhangwa Makoye aliekua
amewawezkea pingamizi Mugosha galibona pamoja na Vedustas Lufano wanaowania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji
ya TFF kupitia kanda ya pili (Mwanza na Mara).
Hata hivyo Paul
Muhangwa Makoye ameweka wazi dhumuni la kusonga mbele katika kamati ya
rufaa, kwa ajili ya kuisaka haki yake ambayo anaiona ni ya msingi kutokana na
maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya uchaguzi.
Wakati huo huo mwenyekiti wa klabu ya Azam FC Said
Muhammed Abeid pamoja na Frank
Mchaki wametangaza hatua ya kuendeleza uhusiano wao wa kuendeleza soka na
kuyaacha masuala yote ya pingamizi baada ya kukutana kwenye kika cha kusikiliza
pingamizi.
Said
Mohamed ambae aliwekewa pingamizi na Frank Mchaki amesema suala hilo kwake limeshamalizika hivyo lililo
mbele yake ni kuendeleza soka.
0 comments:
Post a Comment