Aliekua kocha mkuu wa klabu ya Simba Milovan Circovic, amesema asingependa kuifikisha klabu hiyo mbele
ya shirikisho la soka duniani FIFA, kwa kigezo cha kushindwa kumlipa malipo
anayoudai uongozi wa klabu hiyo baada ya kusitishiwa mkataba wake mwishoni mwa
mwaka 2012.
Milovan
Circovic, ambae yupo nchini tangu juma lililopita kwa ajili ya
kusaka haki yake ambayo aliahidiwa angelipwa mara baada ya fedha za usajili wa
mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel
Okwi zitakapowasili kutoka nchini Tunisia, lakini amesema amekua
akizunguushwa kila anapohitaji msaada wa kukutana na viongozi wa klabu hiyo
kongwe hapa nchini.
Katika hatua nyingine kocha huyo kutoka nchini Serbia
ameonyesha kusikitishwa na mwenendo wa kikosi cha simba tangu alipoondoka
nchini kwa kusema, viongozi wa klabu hiyo wamefanya makosa makubwa kuharibu
mipango aliyokua amejiwekea ndani ya timu hiyo, na matokeo yake hali imeendelea
kuwa mbaya zaidi ya alivyoiacha.
Wakati Milovan
Circovic, akidai kilicho halali kwake kutokana na kusitishiwa mkataba
uongozi wa klabu ya simba umekiri ni kweli unadaiwa na kocha huyo aliewapa
ubingwa msimu wa mwaka 2011-12, lakini wameukana ujio wake kwa kusema
hawakumuarifu aje nchini kwa ajili ya kulipwa pesa zake kwa sasa.
Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema
suala la kocha huyo lipo wazi na kila siku amekua akielezwa kwamba pesa za
usajili wa Emmanuel Okwi
zitakapowasili kutoka nchini Tunisia atalipwa stahiki zake.
Wakati huohuo Uongozi wa klabu ya Simba umekanusha taarifa za kuwa na
mifarakano na baadhi ya wachezaji kama inavyoelezwa katika vyombo mbalimbali
vya habari, hatua mbayo inachukuliwa kama chanzo cha kuendelea kufanya vibaya
katika michezo ya ligi inayowakabili kwa sasa.
Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema hakuna ukweli wa jambo hilo ambalo
limechukua nafasi kubwa katia vyombo vya habari tangu mwishoni mwa juma
lililopita na badala yake kikosi chao kipo katika hali nzuri baada ya kumaliza
mchezo dhidi ya Oljoro JKT ulioshuhudia wakilazimishwa matokeo ya sare ya bao
moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment