Picha na Habari na Yustina David, Mbeya..
Zaidi
ya wanafunzi 70 wa Kidato cha Sita wamehitimu elimu ya juu
ya Sekondari katika shule ya WENDA
HIGH SCHOOL ambapo katika mahafari
hayo wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali.
Akiongea
na wazazi pamoja na wahitimu mgeni rasmi wa mahafari hayo Padre Bazile Mzena
amewahasa wanafunzi hao kumkumbuka Mungu katika masomo yao
ili waweze kufikia malengo yao.
Sherehe
za mahafali ya 4 ya Kidato cha sita shule ya Sekondari Wenda iliyopo Mbalizi zafana viongozi wa
dini wahimiza wanafunzi kujituma katika masomo ya Sayansi.
Wanafunzi
wa Wenda High School wakionesha umahili wao
katika somo la Sayansi ambapo hapa wanaonesha namana walivyobobea katika
uchanganyaji wa kemikamikali.
Mgeni
Rasmi Padre Bazil Mzena ambaye ni mkuu wa Seminary ya Mafinga, akimsikiliza
mwanafunzi wa Wenda
High School aliyekuwa
akimweleza umuhimu wa kujifunza masomo ya Sayansi na matarajio yake mara baada
ya kuhitimu Kidato cha sita.
0 comments:
Post a Comment