Na Ezekiel
Kamanga Mbarali
Mwanamke
aliyefahamika kwa jina la Jerumana Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani
kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya
amedhurumiwa nyumba na serikali ya kijiji hicho.
Hii imekuja
baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka
miwili sasa tangu nyumba yake ya bati ibomolewe ili kupisha shughuli za
kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi kwamba angeweza kujengewa nyumba
nyingine ya kuweza kuishi.
Mjane huyo
ambaye hana watoto amejikuta akiishi kwa dhiki kwa kipindi chote cha
masika ambapo baadhi ya vitu
vimeharibika kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa
kulala
“Mume
wangu alifariki mwaka 2007 na kuanzia mwaka 2010 serikali ya kijiji
imenihamisha na kunileta hapa bila huduma za msingi kama maliwato na
bafu ambapo nimekuwa nikijisetiri
kwa majirani na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza
“ alisema mjane huyo.
Kwa upande wake jirani wa mjane huyo Bwana Mbwiga Mwayila amesema kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha
hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na
hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa adha kwao kwa kuwakatisha usingizi .
Bi Salome
Mwampashi ni jarani wa mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia
haraka mjane huyo ili kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema ameshuhudia
mama huyo akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba
anayoishi kuvuja na moto kuzimika
Naye mwenyekiti
wa kijiji hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwa Fulugence Mhegele amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane
huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta maendeleo ya kijiji ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya
kulipa fidia ingawa diwani huyo
hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo .
0 comments:
Post a Comment