Moto wa mchezo wa hatua ya 16 bora,
unaosubiriwa kwa hamu kubwa na karibu mashabiki wote ulimwenguni kati ya Man
Utd dhidi ya Real Madrid umeanza kuchakata kichwa ni aliekua mshambuliaji wa
mashetani wekundu Cristiano Ronaldo dos
Santos Aveiro baada ya kuuzungumzia kwa hisia
mpambano huo.
Cristiano Ronaldo ambae
kwa sasa ni mshambuliaji wa kutumainiwa wa kikosi cha Real Madrid ameonyesha
hali hiyo kutokana na mazungumzo yake alipohojiwa na vyombo vya habari nchini
Ureno mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 28
amesema ana kikosi cha The merengues kitafanikiwa kuwabwaga Man utd katika
mchezo huo ambao utaanza kuunguruma Estadio Stantiago Bernabeu mnamo Februari
13 kabla ya kumaliziwa huko Old Trafford March 05.
Hata hivyo mshambuliaji huyo ambae
alisajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paundi million 80 iliyoweka rekodi mpaka
sasa ameendelea kusisitiza kwa kusema anatambua Man Utd kwa sasa ndio vinara wa
ligi kuu ya nchini Uingereza na wana timu nzuri, lakini suala hilo haliwatishi
zaidi ya kuamini safari ya kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya
ligi ya mabingwa barani Ulaya ipo mikononi mwao.
Mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya
Man Utd, utakuwa wa kwanza kwa mshambuliaji huyo kukutana na klabu
aliyoitumikia siku za nyuma, na pia mchezo huo utamrejesha kwa mara ya kwanza
katika uwanja wa Old Trafford ambao ulikua kama nyumbani kwake kuanzia mwaka 2003–2009 aliposajiliwa
akitokea Sporting Clube de Portugal ya nchini kwao Ureno.
Wakati huo huo mshambuliaji huyo
amepata wakati mgumu wakati akiripoti kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno,
kufuatia baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo kumkejeli kwa kumuita jina na
Lionel messi ambae kila leo amekua akishindanishwa nae kwenye mijadala ya
kimichezo ama kwenye tuzo za kimataifa.
Hata hivyo Ronaldo hakuonyesha
kuzijali kelele hizo za baadhi ya mashabikia ambao walionekana kuwa na lengo la
kumkejeli baada ya kushindwa na mshambuliaji huyo kutoka nchini Argentina
kwenye ushindani wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.
0 comments:
Post a Comment