Ngassa(Pichani) akiwa mazoezini wakati
Timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS, leo itacheza
mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya waliokua mabingwa wa barani Afrika
mwaka 1984, 1988, 2000 pamoja na 2002 timu ya taifa ya Cameroon.
Mchezo huo unatarajia kuanza majira ya saa kumi na mkoja
jioni katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, unasubhiriwa kwa hamu kubwa
na mashabiki wa soka hapa nchini pamoja na sehemu nyingine za barani Afrika
kufutia mwenendo mzuri wa Taifa Stars ambao walifanikiwa kuwafunga mabingwa wa
Afrika mwaka 2012 timu ya taifa ya zamabia mwishoni mwa mwaka jana.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen amesema
mchezo huo utakua na umuhimu mkubwa kwa kikosi chake ambacho mwezi ujao
kitakabiliwa na mchezo wa kufuzu katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014
dhidi ya timu ya taifa ya morocco.
Kim Paoulsen amesema kikosi chake kipo kamili baada ya kukusanyika
kwa wakati, na pia kipo tayari kuwaikabili timu ya taifa ya Cameroon katika
mchezo wa leo, huku akisisitiza neno umoja ni nguvu kama chagizo la mafanikio
katika mpambano huo
Kwa upande wa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania TAIFA
STARS Juma Kasseja Juma amesema anaamini maandaliozi waliyoyafanya kwa siku
mbili yanakidhi kupambana na kikosi cha Camaroon ambapo hata hivyo amekiri bado
mchezo utakua mgumu baina ya pande zote mbili.
Wakati huo huo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon Jean Paul Akono amesema
mchezo wa leo upo wazi kwa kila mmoja kuchomoza na ushindi kutokana na viwango
vya soka barani Afrika kubadilika kutokana na mazingira ya ushindani yaliopo
kwa sasa.
Akitafsiri yaliyosemwa na kocha huyo kutoka lugha
ya kifaransa, meneja wa The Indomitable Lions Rigobert Song mbae
aliwahi kuwa nahodha wa kikosi cha Cameroon amesema wamekuja nchini kusaka namna ya kujiaandaa
ipasavyo kutokana na uwezo wa timu ya Tanzania kupanda kwa haraka.
Katika hatua nyingine serikali ya jamuhuri ya muungano wa
Tanzania kup[itia wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo imeitakia kila
la kheri Taifa Stars katika mchezo huo muhimu wa kujiandaa na michuano kabambe
inayowakabili kwa ajili ya kupata nafasi ya kushiriki kwenye fainali kubwa
dunia.
Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Fenella Mukangala amesema wapo nyuma ya
timu hiyo kwa kila hali na wanaamini kocha mkuu amekiandaa vyema kikosi chake
kwa ajili ya kupata ushindi.
0 comments:
Post a Comment