Pages


Home » » Kesi inayomkabili Wilvina Mkandara kutokana na kitendo cha kumlisha mtoto kinyesi na kumuunguza mtoto hali iliyomsababishia ulemavu wa mkono ilisikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya .

Kesi inayomkabili Wilvina Mkandara kutokana na kitendo cha kumlisha mtoto kinyesi na kumuunguza mtoto hali iliyomsababishia ulemavu wa mkono ilisikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya .

Kamanga na Matukio | 18:51 | 0 comments
WILVINA MKANDARA  AKIWASONYA NA KUWAKEJELI WAKAZI WA MAJENGO MBEYA WALIOKUJA KUSIKILIZA KESI YAKE KWA KUWAAMBIA MMEACHA KUKAA MAJUMBANI MWENU MMEKUJA KUFUATA UMBEYA TU NIACHENI KUNIFUATAFUATA HUKUMU YA WIL VINA MKANDARA ITATOLEWA  TAREHE 18/2/2013

NA EZEKIEL KAMANGA MBEYA
Kesi inayomkabili Wilvina Mkandara kutokana na kitendo cha kumlisha mtoto kinyesi na kumuunguza mtoto hali iliyomsababishia ulemavu wa mkono ilisikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya
 
Akitoa ushahidi  wake mahakamani mtuhumiwa huyo alikana kuhusika na vitendo hivyo na kudai kuwa mtoto huyo alivunjika alipokuwa akicheza na wenzake na kumpeleka katika hospitali ya Ifisi  ambapo alipewa dawa za kuchua
 
Ushahidi wa  mtuhumiwa huyo ulipingwa na wakili wa serikali Achirey Mulisa na kuitaka mahakama kutupilia mbali vielelezo hivyo vilivyowasilishwa na mtuhumiwa huyo zikiwemo picha na vyeti vya hospitali ya ifisi
 
Hakimu wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo alimuonesha  mtuhumiwa picha za mtoto Aneth baada ya kukatwa mkono na kumuliza anavyojisikia kama mzazi baada ya kuziona picha hizo hali iliyopelekea mtuhumiwa kukaa kimya mahakamani
 
Hata hivyo Kesi hiyo imeahirishwa hadi February 18 mwaka huu  itakapotolewa hukumu 
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger