Shirikisho la Soka Duniani-FIFA
limethibitisha kuwa mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli
unatarajiwa kutumika katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini
Brazil 2014.
Mfumo huo ulitumika kwa mafanikio
katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyofanyika Desemba mwaka jana na pia
itatumika katika michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika Juni mwaka huu.
Rais wa FIFA mara kwa mara amekuwa
akipigia debe mfumo huo toka alipoona bao halali alilofunga kiungo wa Uingereza
Frank Lampard likikataliwa na kupelekea nchi hiyo kufungwa na Ujerumani katika
michuano ya Kombe la Dunia 2010.
FIFA katika mkutano wake wa mwaka
jana ilipitisha mifumo miwili ya Goalref na Hawkeye ambayo yote kwa pamoja
ilitumika katika michuano ya klabu bingwa ya dunia.
0 comments:
Post a Comment