Pages


Home » » Steven George Gerard amewataka mashabiki wa soka nchini England kumuonyesha ushirikiano beki Ashley Cole katika mchi yake ya 100.

Steven George Gerard amewataka mashabiki wa soka nchini England kumuonyesha ushirikiano beki Ashley Cole katika mchi yake ya 100.

Kamanga na Matukio | 03:08 | 0 comments

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Steven George Gerard amewataka mashabiki wa soka nchini humo kumuonyesha ushirikiano beki wa pambeni Ashley Cole endapo atapata nafasi ya kujumuishwa kikosini wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakao unguruma katika uwanja wa Wimbey jijini London dhidi ya mabingwa mara tano wa dunia timu ya taifa ya Brazil.


Steven George Gerard ametoa rai hiyo kwa mashabiki kutokana na Ashely Cole kutarajia kucheza mchezo wa 100 tangu alipoanza kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza mwaka 2001.


Gerard endapo mashabiki watakaojitokeza uwanjani hiyo wataonyesha ushirikiano dhidi ya beki huyo wa klabu ya Chelsea, itakua ni heshima tosha kwake, kutokana na mchango mzuri alio utoa katika timu ya taifa Uingereza ambayo imekikusudia kufikia malengo kwenye michuano ya kimataifa, lakini huwa tofauti.


Katika hatua nyingine beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Uingereza pamoja na klabu ya Liverpool Glen McLeod Cooper Johnson ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwagia sifa kede kede Ashley Cole kwa kusema ni mchezaji mzuri na amekua akijifunza mengi kutoka kwake.


Hata hivyo Glen Johnson ambae aliwahi kucheza sambamba na Ashley Cole wakiwa Chelsea ameungana na Steven George Gerard kwa kuwataka waingereza wote kumpa ushirikiano wa kutosha.




Ashley Cole tangu alipoanza kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza mwaka 2001, amefanikiwa kucheza michezo 99 lakini bado hajafanikiwa kufanga bao hata moja.


Wakati huo huo timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya mwisho ilicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwezi Novemba mwaka 2012, dhidi ya timu ya taifa ya Sweden na kujikuta ikiambulia kisago cha mabao manne kwa mawili, ambapo nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimavic akifunga bao la maajabu.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger